-
Je, mfumo mpya wa kikanda unaofuatiliwa na Iran una sifa gani?
May 23, 2025 23:02Abbas Araghchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amefafanua mfumo mpya wa kieneo unaofuatiliwa na Iran, katika makala iliyochapishwa kwenye tovuti ya Jukwaa la Mazungumzo la Tehran.
-
Khatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Iran haitaachana na haki yake ya teknolojia ya nyuklia
May 23, 2025 08:43Imam wa muda wa Swala ya Ijumaa hapa Tehran amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitasalimu amri na kuachana na haki yake isiyoweza kupokonywa ya matumizi ya amani ya teknolojia ya nyuklia.
-
Iran: Hakutakuwa na makubaliano yoyote iwapo hatutorutubisha wenyewe urani
May 23, 2025 02:58Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran kwa mara nyingine tena amesisitiza kuwa, suala la kurutubisha urani ni mstari mwekundu wa Jamhuri ya Kiislamu katika mazungumzo yajayo ya nyuklia na Marekani na kama Washington itang'ang'ani msimamo wake wa kukataa kurutubishwa urani ndani ya Iran, basi hakuna makubaliano yoyote yatakayofikiwa.
-
Jenerali Baqeri: Vikosi vya Iran havitasita kujibu vitisho vya maadui
May 23, 2025 02:56Mkuu wa Vikosi vya Majeshi ya Iran amesema wanajeshi wa nchi hii hivi sasa wanatengeneza aina mbalimbali za ndege zisizo na rubani na ndege ndogo, akionya kwamba Jamhuri ya Kiislamu itajibu vitisho vyovyote vya maadui kwa jibu lenye mlingano sawa.
-
"Iwapo maadui wangeliamini Iran inaweza kushindwa, wasingejadiliana"
May 22, 2025 23:30Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi amesisitiza kuwa, jukumu la msingi la wizara hiyo ni kujitahidi kuondosha vikwazo na kuongeza kuwa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayesimamia Diplomasia ya Kiuchumi na balozi za Iran nje ya nchi zinapaswa kuwezesha mchakato huo na kuondolewa vikwazo vyote dhidi ya taifa hili.
-
Balozi wa Iran: Tehran yataka kulaaniwa mashambulizi yanayoendelea ya Israel dhidi ya Syria
May 22, 2025 09:09Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa, Amir-Saeed Iravani amesisitiza kuwa, kuendelea mashambulizi ya Israel dhidi ya Syria na kuikalia kwa mabavu Miinuko ya Golan ya Syria na utawala huo ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa na azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
-
Awamu ya tano ya mazungumzo ya Iran na Marekani kufanyika kesho Ijumaa
May 22, 2025 02:38Esmail Baghaei, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, duru ya tano ya mazungumzo yasiyo ya ana kwa ana kati ya Iran na Marekani itafanyika kesho Ijumaa nchini Italia.
-
Bunge: Iran haitakubali kuachia haki yake ya nyuklia
May 22, 2025 00:36Wabunge wa Iran wameendelea kusisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu haitasalimu amri juu ya haki yake ya nyuklia chini ya Mkataba wa Kuzuia Uenezaji wa Silaha za Nyuklia (NPT), hususan haki yake ya kurutubisha urani, huku wakikataa matakwa ya Marekani yaliyowasilishwa kupitia mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja.
-
Pezeshkian: Marekani inafanya uporaji mchana kweupe
May 21, 2025 06:41Rais Masoud Pezeshkian amesema kuwa, rais wa Marekani Donal Trump alisema akiwa nchini Saudia kwamba watu wengine wanapora na kuiba wakati mwenyewe Trump ndiye anayefanya wizi na uporaji mchana kweupe na mbele ya macho ya walimwengu.
-
Bunge lapasisha makubaliano ya kimkakati ya Iran na Russia
May 21, 2025 06:40Wajumbe wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) wamepasisha rasimu ya Mkataba wa Ushirikiano Kamili wa Kimkakati kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Shirikisho la Russia.