-
Khatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Wavamizi watatimuliwa Syria
Dec 13, 2024 06:51Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran ameashiria matukio ya Syria na kusema muqawama utaimarika na kuwatimua waliovamia ardhi ya Syria na kuikalia kwa mabavu.
-
Maonyesho ya bidhaa za Maabara yafunguliwa Tehran
Dec 13, 2024 06:33Maonyesho ya 12 ya Kimataifa ya Vifaa vya Maabara Vilivyotengenezwa nchini Iran yaliyopewa jina la 'IRAN LAB EXPO' yamefunguliwa leo Tehran.
-
Mjumbe wa Iran UN: Mgogoro wa Afghanistan ni shinikizo kwa rasilimali za Iran
Dec 13, 2024 06:31Mjumbe wa Iran katika Umoja wa Mataifa ameikosoa jamii ya kimataifa kwa kushindwa kuiunga mkono Iran licha ya matatizo yanayotokana na mzozo wa nchi jirani ya Afghanistan.
-
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Imarati wazungumza kwa simu kuhusu matukio ya eneo hili
Dec 13, 2024 03:20Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amefanya mazungumzo ya simu na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Muungano wa Falme za Kiarabu na pande mbili zimebadilishana mawazo kuhusu matukio ya eneo hili hususan Syria.
-
Iran yaipongeza IAEA kwa kukiri kuwa Israel ina silaha za nyuklia, yataka ilazimishwe kuharibu silaha hizo
Dec 13, 2024 00:11Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na Masuala ya Kimataifa na Kisheria amejibu hatua ya kukiri Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki kuhusu hatari za silaha za nyuklia za utawala wa Kizayuni, na kuutaka wakala huo ushughulikie silaha za nyuklia za Israel na sio kuusakama mradi wa matumizi ya amani wa nyuklia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Iran na Qatar zasisitiza kuzuiwa mashambulio ya Israel dhidi ya miundomsingi ya Syria
Dec 12, 2024 07:38Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Qatar wamesisitiza juu ya ulazima wa kufanyika juhudi na kuchukuliwa hatua za dhati ili kusimamisha mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya miundomsingi ya Syria na kukalia kwa mabavu maeneo zaidi ya nchi hiyo na utawala huo ghasibu.
-
Vyombo vya Magharibi vyaakisi kwa wingi miongozo ya Kiongozi Muadhamu
Dec 12, 2024 03:01Mashirika ya habari ya nchi za Magharibi yameakisi kwa wingi hotuba na miongozo muhimu ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei aliyotoa jana Jumatano akisisitiza kuwa Marekani na utawala wa Kizayuni ni wahusika wakuu wa matukio ya Syria.
-
Iran yailaani Daesh (ISIS) kwa kumuua waziri wa serikali Taliban Afghanistan
Dec 12, 2024 02:58Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani mauaji ya Khalil-ur-Rehman Haqqani, waziri wa masuala ya wakimbizi wa serikali ya kundi la Taliban nchini Afghanistan.
-
Ndege ya mizigo iliyotengenezwa Iran yafanyiwa majaribio
Dec 12, 2024 00:55Ndege nyepesi ya mizigo ya Iran, iliyopewa jina la Simorgh, ambayo imeundwa kikamilifu na wataalamu wa Kampuni ya Utengenezaji Ndege ya Iran (HESA), imefanyiwa majaribio yaliyofana, baada ya kufanyiwa ukaguzi mbalimbali ili kupokea cheti cha kuraka.
-
Hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu sababu za kuanguka utawala wa Syria
Dec 11, 2024 23:50Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amehutubia hadhara ya matabaka tofauti ya wananchi akigusia matukio ya hivi sasa ya Syria na eneo la Magharibi mwa Asia kwa ujumla, na kueleza sababu za kuanguka utawala wa Syria pamoja na mikakati ya Iran katika kukabiliana na hali ya sasa.