-
Imamu Khamenei: Kilichotokea Syria ni matokeo ya mpango wa pamoja wa Marekani na Israel
Dec 11, 2024 09:07Kiiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, kiilichotokkea Syria ni njama na mpango wa pamoja wa Marekani na utawala haramu wa Israel.
-
Ayatullah Jannati: Marekani na washirika wake lazima wawajibike kuhusu Syria
Dec 11, 2024 09:07Katibu wa Baraza la Kulinda Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Marekani na waitifaki wake wanapaswa kuwajibishwa kuhusiana na matukio ya Syria.
-
Baqaei: Iran inahuisha sentrifyuji zaidi za kisasa katika fremu ya NPT
Dec 11, 2024 03:50Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa uamuzi wa karibuni wa Tehran wa kuhuisha sentrifyuji zaidi za kisiasa umechukuliwa katika fremu ya haki ya nchi wanachama wa mkataba wa NPT na kwa kutolewa taarifa kabla na kwa usimamizi wa Wakala wa kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA).
-
Meja Salami: Iran inafuatilia kwa nguvu zote kuiangusha Israel; nguvu zake haziathiriwi na hali ya Syria
Dec 10, 2024 08:35Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema Iran inafuatilia kwa nguvu zote kuuangusha utawala wa Kizayuni unaoukalia ardhi kwa mabavu na akasisitiza kuwa, vikosi vya ulinzi vya Iran vimeyaweka kwenye nukta ya kuyalenga shabaha maslahi ya kistratejia na muhimu ya maadui katika eneo la Magharibi mwa Asia.
-
Mkuu wa Vyuo vya Kidini akutana na Maulamaa wa Kisunni wa Kurdistan ya Iran, atilia mkazo umoja
Dec 10, 2024 08:34Mkuu wa Vyuo vya Kidini nchini Iran Ayatullah Alireza A'arafi amesisitizia umuhimu wa umoja baina ya nchi za Kiislamu na akasema: kwa kuzingatia hali ya eneo, kujenga umma mmoja na kuwepo umoja baina ya Waislamu ni jambo muhimu zaidi sasa hivi kuliko wakati mwingine wowote.
-
Iran yalaani jinai na uvamizi wa mfululizo wa Israel dhidi ya Syria
Dec 10, 2024 03:03Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani vikali uvamizi na mashambulizi ya mara kwa mara wa utawala wa Kizayuni dhidi ya miundombinu ya Syria ambapo Israel imeteka na kukalia kwa mabavu maeneo mengine ya Syria katika kipindi cha siku chache zilizopita.
-
Iran itajibu hatua za uhasama katika sekta ya nyuklia
Dec 10, 2024 01:02Iran imesisitiza kuwa haitasita kujibu hatua za uhasama zinazolenga mpango wake wa nishati ya nyuklia, lakini bado iko tayari kuendelea na ushirikiano na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA).
-
Spika Qalibaf: Iran itaheshimu uamuzi wowote utakaochukuliwa na watu wa Syria
Dec 09, 2024 23:19Spika wa Bunge la Iran amesema: Jamhuri ya Kiislamu inaheshimu uamuzi wowote utakaochukuliwa na wananchi wa Syria na itaendelea kufuatilia mienendo na sera zake.
-
Baqaei: Jamii ya kimataifa inapaswa kukomesha mauaji ya kimbari ya miaka mia moja huko Palestina
Dec 09, 2024 09:51Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran ameeleza kuwa, utawala ghasibu wa Israel unatumia vibaya hali ya sasa ya Syria ili kuzidisha mauaji ya kimbari huko Gaza na kusema: Jamii ya kimataifa inapapwa kusimama kidete kutetea ubinadamu na kukomesha mauaji ya kimbari ya miaka mia moja yanayoendelea huko Palestina.
-
Stratijia ya kieneo ya Iran, umuhimu wa kuzingatiwa matakwa ya watu wa Syria
Dec 09, 2024 07:07Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inasisitiza juu ya umuhimu wa kuzingatiwa matakwa ya wananchi wa Syria katika mtazamo wake wa kidiplomasia kwa msingi wa matukio yanayojiri hivi sasa katika eneo.