Nchi 35 duniani zinatumia dawa za kibioteknolojia za Iran
(last modified Thu, 06 Feb 2025 02:34:16 GMT )
Feb 06, 2025 02:34 UTC
  • Nchi 35 duniani zinatumia dawa za kibioteknolojia za Iran

Katibu wa Jumuiya ya Watengenezaji na Wasafirishaji wa Bidhaa za Dawa za Sekta ya Bioteknolojia ya Iran ametangaza bidhaa hizo zinauzwa katika nchi 35.

Hossein Amir-Azdi, Katibu wa Jumuiya ya Watengenezaji na Wasafirishaji wa Bidhaa za Kimatibabu za Bioteknolojia ya Iran amesema: Licha ya vikwazo vya kidhalimu vya nchi za Magharibi, sekta ya kibioteknolojia ya dawa ya Iran imeuza nje bidhaa hizo kwa nchi 33 mwaka jana, na kwa nchi 35 mwaka huu."

 Amir Azdi ambaye alikuwa akizungumza mjini Tehran kando ya Kongamano la Nne na Maonyesho ya Dawa za Bioteknolojia na Viwanda Vinavyohusiana ameongeza kuwa: Sekta ya dawa za kibioteknolojia ya Iran inaokoa dola bilioni 2 kwa ajili ya nchi kwa mwaka, na asilimia 60 ya mauzo ya nje ya sekta ya dawa ya Iran yanahusiana na sekta hii.

Katibu wa Jumuiya ya Watengenezaji na Wasafirishaji wa Bidhaa za Dawa za Kibioteknolojia amesema: Leo, kati ya bidhaa 150 za kimataifa za dawa katika uwanja wa biteknolojia, bidhaa 40 zinazalishwa nchini Iran.