Iran ina nafasi muhimu katika soko la kimataifa la teknolojia ya nano
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i122518-iran_ina_nafasi_muhimu_katika_soko_la_kimataifa_la_teknolojia_ya_nano
Katibu wa Taasisi ya Tekenolojia ya Nano ya Iran amesema kuwa, Tehran imekuwa na nafasi muhimu katika soko la kimataifa la teknolojia ya nano kwa kusafirisha bidhaa za nano zenye thamani ya zaidi ya dola milioni moja kwa nchi sita zilizoendelea.
(last modified 2025-02-09T07:11:59+00:00 )
Feb 09, 2025 07:11 UTC
  • Iran ina nafasi muhimu katika soko la kimataifa la teknolojia ya nano

Katibu wa Taasisi ya Tekenolojia ya Nano ya Iran amesema kuwa, Tehran imekuwa na nafasi muhimu katika soko la kimataifa la teknolojia ya nano kwa kusafirisha bidhaa za nano zenye thamani ya zaidi ya dola milioni moja kwa nchi sita zilizoendelea.

Emad Ahmadvand, Katibu wa Taasisi ya Nano ya Iran amesema hayo kujibu swali aliloulizwa kwamba ni nchi gani ni wateja wa teknolojia ya nano ya Iran na kusisitiza kwa kusema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inashiriki kikamilifu katika kuziuzia nano nchi mbalimbali na inashirikiana na nchi 21, 20 na 18 katika nyanja za ujenzi, nguo na zana mbalimbali kwa mpangilio.

Amezitaja nchi sita zilizoendelea ambazo mwaka uliopita zilinunua bidhaa za teknolojia ya nano za Iran kuwa ni Marekani, Russia, Uingereza, China, Korea Kusini na Ujerumani. 

Aidha sambamba na kuashiria kuwa, Iraq ndiyo nchi inayotumia mno bidhaa za teknolojia ya nano za Iran katika nyanja zote za viwanda isipokuwa nyuga chache tu na kuongeza kuwa, katika sekta ya ujenzi, mauzo ya nje ya bidhaa za Iran yamekuwa yakifanyika zaidi katika nchi za Iraq, Afghanistan na Georgia.

Ahmadvand ameongeza kuwa, nchi za India, Pakistan na Imarati (UAE) ndio wanunuzi wakuu wa bidhaa za nanomaterials za Iran kusisitiza kwamba, China na India zinashika nafasi ya kwanza na ya pili katika kununua bidhaa za kemikali za Iran.

Amezungumzia pia bidhaa nyingi za Iran zinazonunuliwa na Uturuki pamoja na nchi za kundi la BRICS.