-
Sisitizo jingine la Iran na Azerbaijan la kutekeleza makubaliano ya nchi mbili
Jun 07, 2024 23:02Katika mazungumzo yake ya simu na Kaimu Rais wa Iran, Mohammad Mokhber, sambamba na kutoa salamu za rambirambi kwa taifa la Iran kutokana na kuondokewa na Rais Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Azerbaijan, Ilham Aliyev, ameeleza mshikamano wake na serikali na wananchi wa Iran.
-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa: Israel imo kwenye maangamizi
Jun 07, 2024 09:25Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema, operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa imeonyesha udhaifu halisi wa utawala wa Kizayuni na imekuwa utangulizi wa kuangamizwa utawala huo.
-
Radiamali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa hatua ya kisiasa na isiyo ya kujenga ya IAEA
Jun 07, 2024 08:30Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeitaja hatua ya Bodi ya Magavana ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ya kuidhinisha azimio jipya dhidi ya Iran kuwa ni hatua ya kisiasa na isiyo ya kujenga.
-
Iran yazitaka nchi za Waislamu kuunganisha nguvu zao kukabiliana na Israel
Jun 07, 2024 02:50Katika mazungumzo ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitizia ulazima wa kuunganishwa nguvu za nchi za Waislamu katika kukabiliana na utawala wa Kizayuni.
-
Kituo kikubwa zaidi cha anga za mbali Asia Magharibi kuanza kazi 2025 Iran
Jun 06, 2024 23:42Ujenzi wa kituo kikubwa zaidi cha anga za mbali katika eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati) unaendelea vizuri hapa nchini Iran, na kinatazimwa kuanza kazi zake mwaka ujao.
-
Iran yajibu ripoti mpya ya IAEA; Tehran italinda haki zake kwa nguvu zote
Jun 06, 2024 06:25Msemaji wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu kamwe haitofumbia macho haki zake za nyuklia na itasimama imara kulinda na kutetea haki zake hizo.
-
IRGC yaiambia Israel: Subirini jibu letu kwa kumwaga damu za wasio na hatia
Jun 06, 2024 00:53Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ametahadharisha kuwa, Israel inapasa kusubiri jibu la Iran kwa kumuua shahidi mmoja wa washauri wa kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu katika uvamizi wa utawala huo wa Kizayuni katika mji wa Aleppo (Halab) huko kaskazini magharibi mwa Syria.
-
Azimio la IAEA halitadhoofisha mipango ya maendeleo ya nyuklia ya Iran
Jun 06, 2024 00:51Wizara ya Mambo ya Nje imelaani vikali hatua ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki, IAEA, ya kupitisha azimio dhidi ya Iran, na kusisitiza kwamba hatua hiyo haitaweza kudhoofisha mipango yake ya maendeleo ya nyuklia.
-
Bagheri Kani katika mkondo wa diplomasia ya muqawama
Jun 05, 2024 09:16Ali Bagheri Kani, Kaimu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika muendelezo wa safari yake ya kieneo jana aliwasili Damascus, mji mkuu wa Syria kwa minajili ya kukutana na kufanya mashauriano na viongozi wa serikali ya nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Iran, China na Russia zazitaka nchi za Magharibi zianze tena kutekeleza makubaliano ya nyuklia
Jun 05, 2024 03:58Iran, China na Russia zimesisitiza kuwa, vifungu vya mkataba wa nyuklia wa JCPOA vingali vina itibari na kuzishauri nchi za Magharibi ambazo zimekwamisha utekelezaji wa mapatano hayo kwa kutochukua hatua na kukhalifu kutekeleza ahadi na majukumu yao, zionyeshe utashi wa kisiasa na kuchukua hatua zinazohitajika ili kuanza kutekeleza tena makubaliano hayo.