Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran kwa mnasaba wa maadhimisho ya " Siku ya Muqawama wa Kiislamu"
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetoa taarifa na kupongeza kuadhimishwa "Siku ya Muqawama wa Kiislamu."
Katika taarifa hiyo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imepongeza maadhimisho ya mwaka wa 18 wa ushindi mkubwa wa wanamapambano fahari wa Kiislamu wa Lebanon katika vita vya siku 33 mwaka 2006 vilivyotoa kipigo cha kihistoria na kuufedhehesha kwa utawala mtendaji jinai, mchokozi na vamizi wa Kizayuni na kueleza kuwa: Agosti 13 ni Siku ya Muqawama wa Kiislamu na kama alivyobainisha Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni siku ambayo muqawama na harakati ya Hizbullah kwa mara nyingine tena ziliurejeshea heshima Ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu.
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imeendelea kubainisha kuwa: Baada ya kupita miaka 18 ya hamasa ya kihistoria ya mapambano na matukio yaliyojiri baada yake khususan oparesheni ya "Kimbunga cha al Aqsa",utawala wa Kizayuni umesajili rekodi ndefu na isiyo ya kifani ya jinai za kivita za kila aina na mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza kwa kusaidiwa na kuungwa mkono kwa pande zote za kisiasa, kiuchumi, kijasusi na kijeshi na serikali ya Marekani na baadhi ya nchi za Magharibi.
Kwa bahati mbaya katika kipindi cha miezi kumi iliyopita dunia imeshuhudia mauaji ya kimbari ya karibu Wapalestina elfu 40 na kujeruhiwa wengine zaidi ya laki moja, kubomolewa miundombinu muhimu na kuwa wakimbizi zaidi ya watu milioni mbili wakazi wa eneo hilo pamoja na mauaji ya kigaidi ya kuvuka mpaka dhidi ya viongozi wa muqawama katika eneo huku taasisi za kimataifa zikinyamaza kimya na kushindwa kuchukua hatua yoyote mkabala wa jinai hizo za Israel.