-
Iran: Msaada wa kimaonyesho wa US kwa Gaza ni mchezo mchungu wa kuigiza
Mar 11, 2024 08:35Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani kile alichokitaja kuwa onyesho chungu la kipropaganda la Marekani na kueleza kuwa, hatua ya Washington ya kudai kuwapa misaada ya kibinadamu Wapalestina wa Gaza, na wakati huo huo inazuia juhudi za kimataifa za usitishaji vita katika eneo hilo lililozingirwa, ni kichekesho.
-
Kufutwa akaunti za mitandao ya kijamii za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi, kielelezo cha uhasama wa Magharibi dhidi ya uhuru wa kusema
Mar 11, 2024 00:52Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema, hatua ya Shirika la Kimarekani la "Meta" (Facebook ya zamani) ya kufuta akaunti za mitandao ya kijamii za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kielelezo cha uhasama na uadui wa Magharibi dhidi ya uhuru wa kusema na kutoa maoni.
-
Iran yasambaratisha mtandao wa Uingereza wa uhalifu wa kifedha na kamari ya intaneti
Mar 10, 2024 03:02Wizara ya Usalama ya Iran imefanikiwa kusambaratisha mtandao mkubwa wa kamari au kubeti kwa njia ya intaneti ambao ulikuwa unaendeshwa na watu wahalifu wakiwa Uingereza.
-
Iran na Oman zataka nchi za Kiislamu kuchukua hatua za kukomesha mauaji ya kimbari Gaza
Mar 09, 2024 23:20Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Oman zimetilia mkazo juu ya udharura wa mataifa ya Kiislamu kuchukua hatua za kukomesha mauaji ya kimbari huko katika Ukanda.
-
Tehran: Taasisi za haki za binadamu za UN ni ‘mwanasesere’ wa baadhi ya tawala za Magharibi
Mar 09, 2024 09:29Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amepinga ripoti ya ujumbe uliopewa mamlaka na Umoja wa Mataifa kuhusu machafuko ya 2022 nchini Iran, akisema kwamba mifumo ya haki za binadamu wa chombo hicho cha kimataifa imegeuka kuwa "mwanasesere" mikononi mwa baadhi ya tawala ili kuendeleza uovu wao.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Hatua ya Meta ya kufuta akaunti za Ayatllah Khamenei ni kinyume cha sheria
Mar 09, 2024 09:28Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amelaani hatua ya kampuni ya Meta ya kuondoa akaunti za Instagram na Facebook za Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei na kusema ni "kinyume cha sheria na na maadili."
-
Rais Raisi: Iran ya leo imeendelea na ni ya teknolojia
Mar 09, 2024 04:13Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Iran ya Kiislamu ya leo imeendelea na ni ya teknolojia.
-
Iran yataka Israel iondolewe kwenye tume ya Umoja wa Mataifa ya haki za wanawake
Mar 09, 2024 02:33Afisa mkuu wa haki za binadamu wa Iran ametoa wito wa kuondolewa utawala haramu wa Israel katika Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya wanawake baada ya maelfu ya wanawake wa Kipalestina kuuawa na kujeruhiwa katika vita vinavyoendelea vya Israel vya mauaji ya kimbari huko Gaza.
-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran: Tuitumie vyema fursa ya mwezi mtukufu wa Ramadhani
Mar 08, 2024 09:16Imam wa muda wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amewataka Waislamu kujiandaa vizuri kwa ajili ya kuingia kwenye mwezi mtukufu wa Ramadhani kama ambavyo pia amesisitiza kwamba, washindi wa vita vya utawala wa Kizayuni huko Ghaza, ni Wapalestina.
-
Iran yaiambia UN: Tuna haki halali ya kujibu vitisho vya Israel
Mar 08, 2024 04:38Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema Jamhuri ya Kiislamu ina kila haki na uhalali wa kuchukua hatua zote inazoweza kujibu uchokozi na tishio lolote kutoka utawala wa Israel dhidi ya usalama wake wa taifa na maslahi ya nchi hii.