-
Shambulio la kigaidi la Israel dhidi ya Syria na kuuawa shahidi washauri watano wa Iran
Jan 21, 2024 05:50Washauri watano wa kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran waliuawa shahidi jana Jumamosi katika shambulizi la kigaidi la anga lililofanywa na utawala wa Kizayuni huko Damascus, mji mkuu wa Syria.
-
Kan'ani: Kuna uhusiano mkubwa kati ya utawala gaidi wa Israel na Daesh
Jan 21, 2024 04:22Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani vikali jinai na uchokozi uliofanywa mapema jana na utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo la raia huko al Mezza, Damascus mji mkuu wa Syria na kuuwa shahidi washauri watano wa kijeshi wa Iran na askari kadhaa wa Syria.
-
Iran na Sudan zatilia mkazo kuiunga mkono Palestina
Jan 21, 2024 04:19Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan wameisitiza ulazima wa kuliunga mkono taifa la Palestina mkabala wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Raisi: Mauaji ya washauri wa kijeshi wa IRGC hayatapita bila kujibiwa
Jan 21, 2024 00:03Rais Ebrahim Raisi wa Iran amelaani vikali shambulizi la kigaidi la Israel katika mji mkuu wa Syria, Damascus lililopelekea kuuawa shahidi washauri watano wa kijeshi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na kusisitiza kuwa, vitendo vya aina hiyo vya kioga haviwezi kupita hivi hivi bila kupewa jibu.
-
Washauri 5 wa Iran wauawa shahidi katika shambulio la kigaidi la Israel huko Damascus
Jan 20, 2024 23:13Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) limetangaza kuwa washauri wake watano wa kijeshi wameuawa katika shambulizi la kigaidi la Israel katika mji mkuu wa Syria.
-
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran: Gaza imekuwa gereza kubwa zaidi la wazi duniani
Jan 20, 2024 10:19Makamu wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika kikao cha Harakati ya Nchi Zisizofungamano ya Siasa za Upande Wowote (NAM) kinachofanyika Kampala nchini Uuganda kwamba: Mzingiro wa muda mrefu wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Ghaza umelifanya eneo hilo kuwa jela kubwa zaidi ya wazi duniani.
-
New York Times: Iran imetuma ujumbe kwa Israel kwa kombora la Khaybar-Shekan
Jan 20, 2024 09:04Gazeti la Marekani la New York Times limelitaja shambulio la hivi karibuni la makombora ya Iran dhidi ya ngome za kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) nchini Syria kwa kutumia kombora la kisasa la "Khaybar Shekan" kuwa sio tu ni kulipiza kisasi dhidi ya ISIS bali pia ni onyesho la nguvu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya kambi ya Magharibi na hasa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Pakistan yatangaza kurejesha uhusiano kamili na Iran baada ya mivutano iliyojitokeza
Jan 20, 2024 03:23Pakistan imetangaza kurejesha kikamilifu uhusiano wa kidiplomasia na Iran baada ya kujitokeza mivutano mikali ya mpakani ambayo haijawahi kushuhudiwa kati ya nchi mbili juu ya operesheni za kupambana na ugaidi.
-
Magaidi kadhaa wa shambulio la Kerman wauawa, baadhi wakamatwa
Jan 20, 2024 00:33Wizara ya Usalama wa Taifa ya Iran imesema vikosi vyake vimefanikiwa kuwaangamiza na kuwatia mbaroni magaidi kadhaa wa shambulio la kigaidi la mapema mwezi huu katika mji wa Kerman, kusini mashariki mwa Iran lililopelekea kuuawa shahidi na kujeruhiwa makumi ya watu.
-
Azma thabiti ya Iran na Pakistan ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kupambana na ugaidi
Jan 19, 2024 23:30Baada ya kushadidi mivutano ya mpakani kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Pakistan katika kipindi cha siku mbili zilizopita, viongozi wa Tehran na Islamabad wamesisitiza kuendeleza uhusiano wa kirafiki kati ya nchi mbili, kuheshimiwa umoja wa ardhi za mataifa hayo mawili na kuwepo uratibu na mashauriano ya karibu zaidi katika kupambana na magenge ya kigaidi.