Apr 14, 2024 07:39 UTC

Wananchi konte nchini Iran wamejitokeza mitaani kuunga mkono hatua ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ya kuuadhibu utawala wa Kizayuni wa Israel kufuatia kitendo chake cha kichokozi cha kutekeleza mashambilizi ya kigaidi dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran jijini Damascus Aprili Mosi.

Baada ya operesheni hiyo iliyofana ya kijeshi ya Iran dhidi ya utawala katili wa Israel mapema leo, wananchi kote Iran wamejitokeza mitaani na kutangaza uungaji mkono wao kwa hatua hiyo ya kijeshi huku wakipiga nara dhidi ya utawala wa Kizayuni. Jijini Tehran umati mkubwa wa watu umeshuhudiwa katika Medani ya Palestina kuunga mkono hatua za kijeshi zilizochukuliwa na Iran.

Wananchi wa Iran ya Kiislamu katika mikoa yote nchini wameungana katika kubainisha furaha yao kufuatia mashambulizi yaliyotekeleza na IRGC dhidi ya utawala wa Israel ambao ni maarufu kwa kuuawa watoto na wanawake wasio na hatia huko Palestina. 

Maandamano pia yamefanyika katika viwanja vya Msikiti wa al-Aqsa katiki mji mkatufu wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na Israel, ambapo Wapalestina walisherehekea baada ya kusikia habari za Iran kutekeleza mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya Israel.

Wanaharakati wanaoiunga mkono Palestina pia wamefanya maandamano mjini Toronto, wakishangilia operesheni hiyo ya kijeshi ya Iran.