-
Rais wa Iran alaani kura ya turufu ya Marekani dhidi ya azimio la UNSC kuhusu Gaza
Dec 10, 2023 23:39Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Ebrahim Raisi ameikosoa Marekani kwa kupinga azimio la Umoja wa Mataifa la kutaka kusitishwa mapigano mara moja kwa sababu za kibinadamu huko Gaza.
-
Droni za Karrar zilizoboreshwa zajiunga na Kikosi cha Anga cha Iran
Dec 10, 2023 06:00Makumi ya ndege zisizo na rubani (droni) aina ya Karrar ambazo zimeboreshwa na kuimarishwa zimejiunga na Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Kan'ani: Marekani, Uingereza na Canada zinapaswa kubebeshwa dhima ya jinai zote za Israel
Dec 10, 2023 05:45Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, tawala za Marekani, Uingereza na Canada zinapaswa kubeba dhima ya jinai zote zinazofanywa na utawala wa Kizayuni kutokana na uungaji mkono mkubwa na wa wazi wa kijeshi, kisiasa, kijasusi na kipropaganda kwa utawala huo dhalimu hasa katika vita vya hivi sasa vya Ghaza.
-
Qalibaf: Muqawama unagawanywa sehemu mbili za kabla na baada ya Kimbunga cha Al Aqsa
Dec 10, 2023 03:24Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesema katika mazungumzo na Waziri Mkuu wa Syria aliyeko ziarani hapa nchini kwamba natija ya oparesheni ya Kimbunga cha Al Aqsa ni nukta adhimu kwa ajili ya harakati ya muqawama kikanda na kimataifa.
-
Raisi: Kimbunga cha al-Aqsa kimepanua mipaka ya muqawama
Dec 10, 2023 00:31Rais wa Iran amesema Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa imepanua mipaka ya muqawama na kuufikisha katika kona zote za dunia.
-
Iran: Operesheni ya Kimbunga cha al Aqsa imeisambaratisha Israel
Dec 09, 2023 11:34Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, operesheni ya Kimbunga cha al Aqsa imeusambaratisha vibaya utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Amir Abdollahian alaani mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni huko Ghaza
Dec 09, 2023 02:55Hossein Amirabdollahian Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran siku ya Ijumaa alilaani mauaji ya halaiki yanayofanywa utawala wa Kizayuni huko katika Ukanda wa Ghaza katika mazungumzo ya simu aliyofanya na Annalena Baerbock, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani.
-
Khatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Wanavyuo wamekuwa mstari wa mbele kupambana na ubeberu wa Marekani
Dec 08, 2023 09:57Imamu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Iran daima wamekuwa mstari wa mbele katika kupambana na ubeberu wa Marekani.
-
Kikosi cha 93 cha Manowari za Jeshi la Iran charejea nyumbani baada ya kulinda doria katika Bahari ya Sham
Dec 08, 2023 04:13Kikosi cha 93 cha Kivita cha Manowari za Kikosi cha Kimkakati cha Wanamaji wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kikiongozwa na manowari ya Jamaran zimerejea nyumbani baada ya siku 102 za kutekeleza jukumu la kuhakikisha usalama wa meli za mafuta na za kibiashara za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Bahari ya Sham na Ghuba ya Aden.
-
Kanani: Baadhi ya wanachama wa G7 ndio chanzo kikuu cha kukosekana utulivu Asia Magharibi
Dec 07, 2023 10:37Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, baadhi ya wanachama wa kundi G7 ndio chanzo kikuu cha ukosefu wa amani na usalama katika Magharibi mwa Asia na duniani.