-
Iran yasema Marekani, E3 zilitumia vibaya IAEA kufikia malengo yao ya kisiasa
Sep 17, 2023 04:25Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema Marekani na nchi tatu za Ulaya katika makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015 zilitumia vibaya Wakala wa Umoja wa Mataifa wa Nishati ya Atomiki kwa madumini ya kufikia malengo yao ya kisiasa.
-
Iran: Tutajibu mapigo ya vikwazo vipya vya Umoja wa Ulaya
Sep 17, 2023 01:08Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu itajibu mapigo kwa hatua ya kujikariri ya Umoja wa Ulaya na Uingereza ya kuendelea kulisakama taifa hili kwa vikwazo.
-
Iran: Mauaji ya kinyama ya Sabra na Shatila ni doa la aibu kwa waungaji mkono wa utawala wa Kizayuni
Sep 16, 2023 08:46Kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mauaji ya Wapalestina wa Sabra na Shatila yaliyofanywa na askari wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameandika ujumbe usemao: Sabra na Shatila daima litabaki kuwa doa la aibu kwenye vipaji vya waungaji mkono wa utawala wa Israel na watetezi wa kizandiki wa haki za binadamu hususan Marekani na Uingereza.
-
Waziri wa Ulinzi wa Iran asema wizi wa mafuta uliofanywa na serikali ya Marekani haukubaliki
Sep 16, 2023 04:39Waziri wa Ulinzi wa Iran amezungumzia hatua ya serikali ya Marekani ya kutwaa meli ya mafuta ya Iran na kupora bidha iliyokuwemo akisema: Hatua ya serikali ya Marekani ni wizi ambao haukubaliwi kwa namna yoyote ile duniani.
-
Ayatullah Khatami: Matembezi ya Arubaini ni shughuli ya kiroho ya aina yake
Sep 15, 2023 08:39Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa hapa Tehran hii leo amesema matembezi ya Arubaini ya Imam Hussein (AS) ni zoezi la kimaanawi la aina yake na lisilo na mfano.
-
Iran: Tutatoa jibu madhubuti kwa vitisho vya Israel
Sep 15, 2023 08:25Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema Jamhuri ya Kiislamu itatoa jibu madhubuti kwa vitisho vyovyote na vitendo haramu vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya taifa hili.
-
Qatar: Kutumwa pesa za Iran zilizoshikiliwa Korea Kusini kutamalizika wiki ijayo
Sep 15, 2023 04:43Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar, Sheikh Mohammed Bin Abdulrahman al-Thani, amesema kuwa mchakato wa kutuma fedha za Iran zilizokuwa zinashikiliwa nchini Korea Kusini kwenye akaunti za benki nchini Qatar kutamalizika wiki ijayo.
-
Iran yakosoa uamuzi wa nchi 3 za Ulaya wa kuendeleza vikwazo
Sep 15, 2023 04:19Iran imelaani uamuzi wa Uingereza, Ufaransa na Ujerumani (E3) wa kuendeleza vikwazo vyao vya makombora ya balistiki na vinavyohusiana na nyuklia dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kinyume na makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015 kati ya Tehran na madola sita makubwa ya dunia.
-
Salami: Vitisho dhidi ya Iran vinazidi kufupisha uhai wa Israel
Sep 14, 2023 23:55Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ameionya Israel na kusema kuwa, vitisho vya Tel Aviv dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran havitakuwa na matokeo mengine isipokuwa kuendelea kufupisha uhai wa utawala wa Kizayuni.
-
Sisitizo la Iran la kutekelezwa makubaliano ya usalama na Iraq
Sep 14, 2023 10:48Akizungumza tarehe 11 Septemba hapa mjini Tehran na Bafel Talabani, Mkuu wa Muungano wa Kizalendo wa Kurdistan ya Iraq, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya ametaka makubaliano ya usalama yaliyofikiwa kati ya Iran na Iraq yatekelezwe haraka iwezekanavyo.