-
Kamanda Hajizadeh: Kombora la Hypersonic litazinduliwa hivi karibuni
May 29, 2023 22:08Kamanda wa Kikosi cha Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, SEPAH, amesisitiza kuwa: Kombora la balistiki la Hypersonic la Iran litazinduliwa hivi karibuni.
-
Iran yasema iko tayari kujiunga na kundi la "BRICS"
May 29, 2023 22:07Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Anayeshughulikia Diplmasia ya Uchumi amesisitiza kuwa Iran iko tayari kuwa mwanachama wa kundi la BRICS.
-
Kiongozi Muadhamu: Iran inakaribisha kuhuishwa uhusiano wake na Misri
May 29, 2023 08:02Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema Iran inakaribisha azma ya kufufuliwa uhusiano wake na Misri.
-
Sultan Haitham aonana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
May 29, 2023 03:52Sultan Haitham bin Tariq Aal Saeed wa Oman na ujumbe alioandamana nao wameonana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei hapa Tehran.
-
Rais wa Iran ampongeza Recep Tayyip Erdogan kwa kuchaguliwa tena kuongoza Uturuki
May 29, 2023 02:23Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma pongeza kwa Rais Recep Tayyip Erdogan kwa kuchaguliwa tena kuongoza Uturuki na kusema kuwa, huo ni ushahidi kwamba wananchi wa nchi hiyo bado wanamwamini.
-
Wagonjwa milioni 1.2 wa kigeni watibiwa katika hospitali za Iran
May 29, 2023 02:21Waziri wa Afya wa Iran Bahram Einollahi anasema kuwa nchi yake imepata maendeleo makubwa katika sekta ya afya tangu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979, na kuongeza kuwa zaidi ya wagonjwa milioni 1.2 wa kigeni walitibiwa katika hospitali za Iran mwaka jana.
-
Iran: Uhusiano wetu na Oman umezidi kustawi kutoka hatua ya biashara hadi hatua ya uwekezaji
May 28, 2023 22:37Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, uhusiano wetu na Oman umestawi zaidi hivi sasa na umefikia hatua ya uwekezaji kutoka hatua ya kibiashara. Mitazamo ya pande mbili pia ya kuimarisha mshikamano wa kikanda wa viongozi wa nchi hizo mbili nao umezidi kuimarika.
-
Sultani Haitham wa Oman awasili nchini na kulakiwa rasmi na Rais Raisi
May 28, 2023 10:57Hafla rasmi ya kumkaribisha Sultani Haitham Bin Tariq Al Saeed wa Oman, ambaye ametembelea Iran kwa mara ya kwanza akiwa Mfalme wa Oman, imefanyika katika jumba la kiutamaduni na kihistoria la Saad Abad hapa mjini Tehran.
-
Idadi ya watalii wanaoitembelea Iran yaongezeka kwa asilimia 300
May 28, 2023 03:28Shirika la Kimataifa la Utalii la Umoja wa Mataifa (UNWTO) limesema zaidi ya watalii milioni 4.1 waliitembelea Iran mwaka jana 2022, hilo likiwa ni ongezeko la asilimia 315 ikilinganishwa na mwaka juzi 2021.
-
Rais wa Iran: Wanachama wa OPEC waungane kuzuia migawanyiko inayoibuliwa na Wamagharibi
May 28, 2023 00:16Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na Katibu Mkuu wa Shirika la Nchi Zinazouza Mafuta Kwa Wingi Duniani (OPEC) na kusema: "Nchi wanachama wa OPEC ziungane ili kuzuia njama za Wamagharibi za kuibua hitilafu katika shirika hilo."