Sultan Haitham aonana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
May 29, 2023 03:52 UTC
Sultan Haitham bin Tariq Aal Saeed wa Oman na ujumbe alioandamana nao wameonana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei hapa Tehran.
Katika mazungumzo hayo, Rais Ebrahim Raisi ameandamana na Sultan Haitham ambaye yupo hapa nchini Iran kwa ziara rasmi ya siku mbili.
Hii ni ziara ya kwanza rasmi ya Sultan Haitham kuitembelea Iran tangu alipochukua cheo hicho.
Maelezo zaidi kuhusu habari hiyo yatakujieni katika matangazo yajayo ya Idhaa ya Kiswahili, Radio Tehran.