-
Iran yajibu uvumi wa gazeti la Marekani kuhusu kuishambulia Saudia
Nov 02, 2022 23:11Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amejibu uvumi ulioenezwa na gazeti la Marekani la Wall Street Journal lililodai kuwa kuna uwezekano Iran ikashambulia baadhi ya maeneo ya Saudi Arabia na kusema kuwa hayo ni madai chapwa yasiyo na msingi wowote.
-
Kiongozi Muadhamu: Tarehe 13 Aban inadhihirisha uovu, ukhabithi na kushindwa Marekani
Nov 02, 2022 10:14Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, tarehe 13 Aban (Novemba 4) ni mfano wa wazi wa uovu, ukhabithi na dhihirisho la kupata pigo na kushindwa Marekani.
-
Eslami: Mafaili ya madai dhidi ya Iran yanapasa kufungwa na vikwazo viondolewe
Nov 01, 2022 23:17Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amesisitiza ulazima wa kufungwa mafaili ya madai yaliyotolewa dhidi ya miradi ya kuzalisha nishati ya nyuklia ya Jamhuri ya Kiislamu na kuondolewa vikwazo.
-
Iran yajitosheleza katika uzalishaji wa bidhaa 500 za tiba
Nov 01, 2022 07:58Msemaji wa serikali ya Iran amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu imeweza kujitosheleza katika uzalishaji wa bidhaa 500 tofauti za tiba.
-
Iran yawawekea vikwazo shakhsia 10 na taasisi nne za Marekani
Nov 01, 2022 04:10Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa imeyaweka majina ya shakhsia kumi na taasisi nne za Marekani kwenye orodha yake ya vikwazo.
-
Meli ya kigeni yakamatwa Ghuba ya Uajemi ikisafirisha kimagendo lita milioni 11 za mafuta
Oct 31, 2022 23:14Afisa wa ngazi za juu wa Idara ya Mahakama ya Iran amesema, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limeinasa meli ya kigeni ya mizigo iliyokuwa imebeba mamilioni ya lita za mafuta yanayosafirishwa kimagendo katika maji ya Ghuba ya Uajemi na kuwakamata pia wafanyakazi wote wa meli hiyo.
-
Watu 6 katika timu ya magaidi watenda jinai katika Haramu takatifu ya Shah Cheragh watiwa nguvuni
Oct 31, 2022 08:48Wizara ya Intelijinsia ya Iran imetangaza kuwa, imewatambua na kuwatia nguvuni watu sita katika timu ya usaidizi ya magaidi watenda jinai dhidi ya Haram takatifu ya Ahmad bin Musa (as) huko katika mji wa Shiraz.
-
Rais Raisi: Usalama wa Iran ni mstari mwekundu
Oct 31, 2022 04:03Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Ebrahim Raeisi amesema usalama ni mstari mwekundu kwa serikali yake na kwamba haitaruhusu maadui kuudhoofisha.
-
Kamanda wa IRGC: Tutaharibu usalama wa yeyote atakayedhuru usalama wa Iran
Oct 31, 2022 03:39Kamanda wa Kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ametoa onyo kali kwa maadui, akisema kuwa vikosi vya Iran havina kikomo linapokuja suala la kulinda usalama wa nchi.
-
Raia wa Iran wamewaaga mara ya mwisho mashahidi wa hujuma ya kigaidi ya Shah Cheragh
Oct 31, 2022 01:22Raia wa Iran wameshiriki katika hafla tofauti za maombolezo na maziko kote nchini ili kuwaaga baadhi ya mashahidi wa shambulio la kigaidi kwenye Haram Tukufu ya Shah Cheragh ya mjini Shiraz, kusini magharibi mwa Iran.