-
Iran yazindua droni yake ya Ghaza na mafanikio yake mapya ya kijeshi
May 21, 2021 08:28Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezindua mafanikio matatu makubwa ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ikiwemo droni (ndege isiyo na rubani) ya Ghaza.
-
Zarif: Kuendelezwa vikwazo vya Trump kama silaha katika mazungumzo, hakukubaliki
May 21, 2021 08:27Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaumu kitendo cha Marekani ya kuendelea na vikwazo haramu na visivyo na chembe ya ubinadamu vilivyowekwa na Donald Trump dhidi ya taifa la Iran na kusema kuwa kitendo hicho hakikubaliki hata kidogo.
-
Zarif: Uvamizi wa Israel umethibitisha kwamba, kuanzisha uhusiano na Israel hakuna faida
May 21, 2021 03:46Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza haki ya Wapalestina ya kujitetea mbele ya dhulma na ukandamizaji wa utawala wa kiapathaidi wa Israel na kusema kuwa, kuporwa na kughusubiwa kitongoji kingine cha Waarabu pambizoni mwa Msikiti wa al-Aqswa kumethibitisha kwamba, kuanzisha uhusiano wa kawaida baadhi ya nchi za Kiarabu na Israel hakuna faida yoyote.
-
Ayatullah Makarim: Wazayuni wameionyesha dunia hulka yao ya ushenzi
May 20, 2021 23:07Ayatullah Nasir makarim Shirazi, mmoja wa Marjaa Taqlidi aliyeko mji mtukufu wa Qum amelaani hatua za kinyama zinazochukuliwa na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel za kuua na kumwaga damu za wanaume, wanawake na watoto madhulumu na wasio na ulinzi wa Palestina.
-
Rais Rouhani: Vikwazo haviwezi kuikwamisha Iran kujiletea maendeleo
May 20, 2021 07:20Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya iran amesema kuwa, kuzinduliwa miradi mikubwa ya kitaifa ya petrokemikali ni uthibitisho wa wazi kuwa, taifa la Iran limesimama imara na kwamba vikwazo na mashinikizo ya kiuchumi hayawezi kulikwamisha taifa hili katika jitihada zake za kujiletea maendeleo.
-
Salami: Iran itaendelea kuunga mkono taifa la Palestina
May 20, 2021 03:29Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Iran (IRGC) Meja Jenerali Hossein Salami amesema Iran itaendelea kuunga mkono taifa la Palestina.
-
Duru ya nne ya mazungumzo ya Vienna; kupiga hatua katika kivuli cha baadhi ya hitilafu
May 20, 2021 02:41Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amesema mwishoni mwa duru ya nne ya mazungumzo ya Vienna, Austria kwamba, kumepigwa hatua nzuri katika mazungumzo hayo ya nyuklia, lakini bado haiwezekani kusema kwamba, kila kitu kimemalizika.
-
Maandamano yafanyika Tehran kulaani jinai za utawala wa Israel huko Ghaza
May 19, 2021 22:04Maandamano yamefanyika mjini Tehran kulaani jinai zinazoendelea kufanywa na utawala katili wa Israel dhidi ya Wapalestina wasio na hatia katika Ukanda wa Ghaza.
-
Rouhani: Uchaguzi wa rais Iran unaangaziwa kimataifa
May 19, 2021 21:54Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema macho ya dunia yameelekezwa kwenye uchaguzi ujao wa rais nchini Iran.
-
Spika wa Bunge la Iran akosoa kimya cha jamii ya kimataifa kwa jinai za Israel
May 19, 2021 06:55Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa vikali kimya cha jamii ya kimataifa , asasi za kibinadamu na Umoja wa Mataifa kwa jinai za utawala haramu wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina.