Ayatullah Makarim: Wazayuni wameionyesha dunia hulka yao ya ushenzi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i70372-ayatullah_makarim_wazayuni_wameionyesha_dunia_hulka_yao_ya_ushenzi
Ayatullah Nasir makarim Shirazi, mmoja wa Marjaa Taqlidi aliyeko mji mtukufu wa Qum amelaani hatua za kinyama zinazochukuliwa na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel za kuua na kumwaga damu za wanaume, wanawake na watoto madhulumu na wasio na ulinzi wa Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 20, 2021 23:07 UTC
  • Ayatullah Makarim: Wazayuni wameionyesha dunia hulka yao ya ushenzi

Ayatullah Nasir makarim Shirazi, mmoja wa Marjaa Taqlidi aliyeko mji mtukufu wa Qum amelaani hatua za kinyama zinazochukuliwa na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel za kuua na kumwaga damu za wanaume, wanawake na watoto madhulumu na wasio na ulinzi wa Palestina.

Ayatullah Makarim ameeleza katika taarifa kwamba, mbele ya kimya cha jamii ya kimataifa, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na wengineo wanaojigamba kuwa watetezi wa haki za binadamu, utawala katili wa kizayuni umeonyesha hulka na dhati yake halisi ya kishenzi kwa kuua na kumwaga damu za wanaume, wanawake na watoto madhulumu na wasio na ulinzi wa Palestina.

Katika sehemu nyingine ya taarifa yake,  Alimu huyo wa juu wa kidini amesema: Mbali na kulaani jinai za utawala wa Kizayuni na kuzifariji familia za mashahidi, majeruhi na waliopoteza makazi yao, nawapa heko wanamapambano shujaa wa Palestina kwa hima na jujhidi zao za kupigania ukombozi wa Quds tukufu kutoka kwenye makucha ya uvamizi wa Wazayuni.

Wanamapambano wa Palestina

Uvamizi na mashambulio makubwa na ya kinyama ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza leo Ijumaa yameingia siku yake ya 11.

Kwa mujibu wa wizara ya afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza, tangu yalipoanza mashambulio hayo hadi sasa, Wapalestina wasiopungua 230 wakiwemo watoto 65 wameuawa shahidi na wengine zaidi ya 1,600 wamejeruhiwa.../