Rais Rouhani: Vikwazo haviwezi kuikwamisha Iran kujiletea maendeleo
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i70354-rais_rouhani_vikwazo_haviwezi_kuikwamisha_iran_kujiletea_maendeleo
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya iran amesema kuwa, kuzinduliwa miradi mikubwa ya kitaifa ya petrokemikali ni uthibitisho wa wazi kuwa, taifa la Iran limesimama imara na kwamba vikwazo na mashinikizo ya kiuchumi hayawezi kulikwamisha taifa hili katika jitihada zake za kujiletea maendeleo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 20, 2021 07:20 UTC
  • Rais Rouhani: Vikwazo haviwezi kuikwamisha Iran kujiletea maendeleo

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya iran amesema kuwa, kuzinduliwa miradi mikubwa ya kitaifa ya petrokemikali ni uthibitisho wa wazi kuwa, taifa la Iran limesimama imara na kwamba vikwazo na mashinikizo ya kiuchumi hayawezi kulikwamisha taifa hili katika jitihada zake za kujiletea maendeleo.

Rais Hassan Rouhani amesema hayo leo Alkhamisi na kuongeza kuwa, kuzinduliwa miradi 17 mikubwa ya petrokemikali katika kipindi cha mwaka mmoja lilikuwa ni jambo zito sana, lakini leo hii, suala hilo limewezekana.

Amesema, serikali yake imeweza kupata mafanikio makubwa katika sekta ya prokemikali kwa maana halisi ya neno na leo hii uwezo wa sekta hiyo nchini Iran umepanda kutoka kuzalisha tani milioni 56 hadi tani milioni 100; na hiyo ni fakhari kubwa ya kujivunia.

Amesema, katika kipindi cha miaka minane iliiyopita, dola bilioni 130 zimeongezeka katika bidhaa zisizo za mafuta zinazosafirishwa nje ya Iran na inapolinganishwa na miaka minane ya kabla yake, tutaona kuwa, usafirishaji nje bidhaa zisizo za mafuta za Iran, umeongezeka kwa takriban asilimia 59.

Uchumi wa muqawama wa Iran

 

Rais Rouhani aidha amesema, katika kipindi cha miezi miwili, mitatu iliyopita, serikali yake imejikita zaidi katika kutatua masuala mawili makuu, janga la corona na vikwazo na kwa uwezo na taufiki ya Mwenyezi Mungu, tutazishinda tu changamoto hizo mbili.

Amesema, anatoa ahadi hizo kwa kuzingatia kuwa, katika mazungumzo ya Vienna, upande wa pili wa makublaiano ya JCPOA umeshakubali kuondoa vikwazo vikuu, kuanzia vya sekta ya mafuta na petrokemikali hadi vya bima, Benki Kuu na usafiri wa majini.

Leo Rais Rouhani amezindua kwa njia ya video, miradi mikubwa ya kitaifa ya petrokemikali ambayo imefanikishwa kwa gharama ya dola bilioni moja na milioni 304.