-
Hatima ya JCPOA kupitia mazungumzo ya Vienna
Apr 19, 2021 07:10Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imechukua maamuzi na kutekeleza hatua za kujibu mapigo, kutokana na Marekani kujitoa kwenye makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kwa kufuata sheria ya “hatua ya kimkakati kwa ajili ya kuondolewa vikwazo na kulindwa maslahi ya taifa la Iran”.
-
Kiongozi Muadhamu asikitishwa na kifo cha Shahidi Jenerali Hijazi
Apr 19, 2021 03:20Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa mkono wa pole na kueleza juu ya kusikitishwa kwake na kifo cha Brigedia Jenerali Mohammad Hosseinzadeh Hijazi, Naibu Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ambaye ameaga dunia usiku wa kuamkia leo akiwa na umri wa miaka 65, kutokana na mshtuko wa moyo.
-
Iran yaomboleza kifo cha Naibu Kamanda wa Kikosi cha Quds cha IRGC
Apr 19, 2021 03:19Naibu Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) ameaga dunia.
-
Rouhani: Taifa la Zimbabwe litavishinda vikwazo vya Marekani
Apr 18, 2021 22:24Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemtumia ujumbe wa pongezi mwenzake wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa kwa mnasaba wa Siku ya Uhuru wa nchi hiyo ya kusini mwa Afrika, iliyoadhimishwa jana Jumapili.
-
Iran: Kurutubisha urani kwa 60% ni jibu kwa njama za maadui
Apr 18, 2021 22:24Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema urutubishaji wa madini ya urani kwa kiwango cha asilimia 60 hapa nchini ni jibu kwa njama na chokochoko za maadui wa taifa hili.
-
Rais Hassan Rouhani asisitiza kupanuliwa ushirikiano wa Iran na Serbia
Apr 18, 2021 07:50Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya udharura wa kupanuliwa ushirikiano kati ya taifa hili na Serbia.
-
Watu 405 waripotiwa kufariki duniani nchini Iran kwa Covid-19
Apr 18, 2021 07:46Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran amesema kuwa, watu 405 wamefariki dunia kwa Covid-19 nchini Iran katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita na kuifanya idadi ya watu walioaga dunia hadi sasa kwa virusi hivyo hapa nchini kufikia 66,732.
-
Urutubishaji wa madini ya urani hadi asilimia 60 nchini Iran na kelele za kisiasa zilizoibuliwa
Apr 18, 2021 06:19Iran kamwe haifuatilii shughuli zisizo za kawaida za nyuklia na wala haina mpango wa kutengeneza silaha za nyuklia. Huu ni ukweli ambao umethibitishwa mara kadhaa katika ripoti za Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA).
-
Iran yazindua mitambo mipya kabisa ya makombora katika gwaride la "Siku ya Jeshi"
Apr 18, 2021 03:36Mitambo mipya kabisa ya makombora ya vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezinduliwa katika gwaride maalum lililofanyika mapema leo kwa mnasaba wa "Siku ya Jeshi".
-
Araqchi: Tumeingia kwenye mkondo sahihi wa mazungumzo ya JCPOA
Apr 17, 2021 22:27Sayyid Abbas Araqchi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika masuala ya kisiasa amesema baada ya kikao cha kamati ya pamoja ya mapatano ya nyuklia ya JCPOA mjini Vienna, Austria kwamba inavyoonekana sasa tumeingia katika mkondo sahihi wa mazungumzo hayo baada ya siku kadhaa za majadiliano mazito ingawa hata hivyo bado kuna safari ndefu mbele yetu.