Iran yaomboleza kifo cha Naibu Kamanda wa Kikosi cha Quds cha IRGC
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i69206-iran_yaomboleza_kifo_cha_naibu_kamanda_wa_kikosi_cha_quds_cha_irgc
Naibu Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) ameaga dunia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 19, 2021 03:19 UTC
  • Iran yaomboleza kifo cha Naibu Kamanda wa Kikosi cha Quds cha IRGC

Naibu Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) ameaga dunia.

Msemaji wa IRGC, Ramezan Sharif amesema Brigedia Jenerali Mohammad Hosseinzadeh Hijazi, Naibu Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ameaga dunia usiku wa kuamkia leo akiwa na umri wa miaka 65, kutokana na mshtuko wa moyo.

Ameongeza kuwa, Shahidi Hijazi ameaga dunia kutokana na athari za kemikali zilizomuingia mwilini wakati wa Vita vya Kujihamu Kutakatifu vilivyoanzishwa na Iraq dhidi ya Iran katika miaka 80.

Msemaji wa SEPAH amebainisha kuwa, Brigedia Jenerali Hijazi alikumbwa na ugonjwa wa Covid-19 miezi kadhaa iliyopita. Shahidi Hijazi alikuwa mmoja wa maveterani waliopigana mstari wa mbele katika vita vya kichokozi vilivyoanzishwa na aliyekuwa dikteta wa Iraq, Saddam Hussein kuanzia mwaka 1980 hadi 1988.

Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon (kulia) amuomboleza Shahidi Hijazi

Risala za rambirambi zinaendelea kutumwa kwa familia, jamaa na mafariki wa marehemu Shahidi Hijazi ambaye anatazamiwa kuzikwa leo Jumatatu.

Miongoni mwa viongozi na maafisa wa Iran waliotoa mkono wa pole ni Spika wa Bunge la Iran, Mohammad-Baqer Qalibaf, Mkuu wa Vyombo vya Mahakama, Ibrahim Raesi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Muhammad Javad Zarif miongoni mwa maafisa wengine wa ngazi za juu.