Watu 405 waripotiwa kufariki duniani nchini Iran kwa Covid-19
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i69176-watu_405_waripotiwa_kufariki_duniani_nchini_iran_kwa_covid_19
Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran amesema kuwa, watu 405 wamefariki dunia kwa Covid-19 nchini Iran katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita na kuifanya idadi ya watu walioaga dunia hadi sasa kwa virusi hivyo hapa nchini kufikia 66,732.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 18, 2021 07:46 UTC
  • Watu 405 waripotiwa kufariki duniani nchini Iran kwa Covid-19

Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran amesema kuwa, watu 405 wamefariki dunia kwa Covid-19 nchini Iran katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita na kuifanya idadi ya watu walioaga dunia hadi sasa kwa virusi hivyo hapa nchini kufikia 66,732.

Kitengo cha Mahusiano ya Umma cha Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran kimetangaza kuwa, kwa mujibu wa matokeo ya vipimo rasmi walivyofanyiwa watu  katika muda wa masaa 24 yaliyopita wagonjwa wapya 21,644 waliokumbwa na ugonjwa wa COVID-19 wamegunduliwa humu nchini, ambapo 3,092 miongoni mwao wamelazwa hospitalini na waliobakia wamepatiwa huduma za tiba na kuruhusiwa kurudi nyumbani.

Kadhalika taarifa ya Kitengo cha Mahusiano ya Umma cha Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran  imesema kuwa, idadi ya watu waliogunduliwa kupatwa na ugonjwa wa COVID-19 nchini Iran hadi hivi sasa imefikia 2,237,089.

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imesema kuwa, hadi hivi sasa wagonjwa milioni mbili na laki 7 na 85,358 wameshapata afueni kikamilifu baada ya kuugua ugonjwa huo nchini Iran na wameruhusiwa kurudi nyumbani. 

 

Wakati huo huo, Idadi ya wagonjwa waliofariki dunia kutokana na ugonjwa wa corona ulimwenguni imepindukia milioni 3.

Marekani imeendelea kuwa nchi iliyoathiriwa zaidi na maambukizo na vifo vya corona ambapo karibu watu 600,000 wameaga dunia kwa maradhi hayo katika nchi hiyo.

Nchi 10 zinazoifuatia Marekani kwa idadi kubwa ya wagonjwa wa COVID-19 ni India, Brazil, Ufaransa, Russia, Uingereza, Uturuki, Italia, Uhispania, Ujerumani na Poland.