Rais Hassan Rouhani asisitiza kupanuliwa ushirikiano wa Iran na Serbia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i69184-rais_hassan_rouhani_asisitiza_kupanuliwa_ushirikiano_wa_iran_na_serbia
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya udharura wa kupanuliwa ushirikiano kati ya taifa hili na Serbia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 18, 2021 07:50 UTC
  • Rais Hassan Rouhani asisitiza kupanuliwa ushirikiano wa Iran na Serbia

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya udharura wa kupanuliwa ushirikiano kati ya taifa hili na Serbia.

Rais Rouhani amesisitiza hilo katika mazungumzo yake leo hapa mjini Tehran na Nikola Selakovic, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Serbia na kueleza kwamba, siku zote Iran imekuwa ikisisitiza umoja wa kitaifa wa Serbia.

Rais Rouhani sambamba na kubainisha kwamba, Iran inaamini suala la udharura wa kulindwa usalama, amani na uthabiti katika eneo la Balkan na kuishi kwa amani na salama kaumu na jamii zote na kuongeza kuwa, vita dhidi ya ugaidi na kurejesha amani na usalama kunahitajia ushirikiano na juhudi za pande zote za mataifa ya dunia.

 Mazungumzo ya Rais Hassan Rouhani na Nikola Selakovic, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Serbia (Jumapili, 18.04.2021)

 

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria pia vikwazo vya kidhalimu na vita vya kiuchumi vya miaka mitatu vya Marekani dhidi ya taifa hili na kueleza kwamba, kuondolewa kikamilifu vikwazo hivyo kutapelekea kupatikana anga mpya kwa ajili ya ushirikiano wa kiuchumi wa Iran na mataifa ya dunia; na kwamba, ni bora kwa mataifa rafiki yakafanya juhudi za kunufaika na fursa hii.

Kwa upande wake, Nikola Selakovic Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Serbia amesema kuwa, daima nchi yake imekuwa na azma ya kuwa na uhusiano wa kirafiki na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kwamba, ina hamu na shauku ya kupanuliwa zaidi ushirikiano wa pande mbili katika nyanja mbalimbali.