-
Iran yalaani kufunguliwa ubalozi wa Bahrain mjini Tel Aviv
Apr 04, 2021 03:25Kongamano la Kimataifa la Kuunga Mkono Intifadha ya Palestina katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, limelaani hatua ya utawala wa kifalme wa Bahrain kufungua ubalozi katika utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Sheikh Shahriyari: Waislamu wafanye juhudi za kusambaratisha siasa za kuwafarakanisha
Apr 03, 2021 22:36Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu amesema kuwa, hii leo Ulimwengu wa Kiislamu unahitajia kuliko wakati mwingine wowote juhudi za kuondoa mapengo na mifarakano inayopandikizwa na maadui.
-
Msimamo wa Iran kuhusu taarifa ya pamoja ya JCPOA
Apr 03, 2021 05:35Jamhuri ya Kiislamu haitakubali mpango wowote wa kuondolewa vikwazo vikwazo vya Marekani hatua kwa hatua.
-
Salehi: Mkwamo katika mapatano ya JCPOA umeanza kuondoka
Apr 03, 2021 02:58Mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Iran amesema kuwa, mkwamo katika mapatano ya kimataifa ya nyuklia ya JCPOA umeanza kuondoka na kuongeza kuwa, kwa vile hivi sasa mazungumzo kuhusu JCPOA yameingia katika hatua ya kiufundi na yameshatoka kwenye mivutano ya awali, maana yake ni kwamba mkwamo katika mazungumzo hayo umeanza kuondoka.
-
Zarif: Hakuna udharura wa kufanyika mkutano kati ya Iran na Marekani
Apr 02, 2021 22:10Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema hakuna mazungumzo yoyote yatakayofanyika baina ya Jamhuri ya Kiislamu na Marekani juu ya kuhuisha makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, na kwamba hakuna udharura wa kufanyika mkutano baina Tehran na Washington.
-
Araqchi: Kuondolewa vikwazo na Marekani ndio hatua ya kwanza ya kufufua JCPOA
Apr 02, 2021 09:51Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amesema, kuondolewa vikwazo na Marekani ndio hatua ya kwanza ya kufufua makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Baraza la Kukurubisha Madhehebu lapongezwa kwa kuimarisha umoja baina ya Waislamu
Apr 02, 2021 09:41Katibu Mkuu wa Harakati ya Umma ya Lebanon ametilia mkazo nafasi ya Baraza la Kimataifa la Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu katika kuimarisha umoja baina ya Waislamu.
-
Namaki: Iran itakuwa moja ya vituo vikuu vya uzalishaji wa chanjo duniani
Apr 02, 2021 02:06Waziri wa Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu wa Iran amesema kuwa, kutokana na hima ya vijana wa nchi hii, Iran itakuwa moja ya wazalishaji wakuu wa chanjo ya corona ulimwenguni.
-
Zarif: Hati ya ushirikiano kati ya Iran na China haihitaji kupasishwa na bunge
Apr 01, 2021 22:50Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amefafanua kuhusu mpango wa ushirikiano wa pande zote kati ya Iran na China na kuandika kuwa: hati hiyo haihitajii kupasishwa na Majlisi ya Ushuari ya Kiislamu ya Iran (Bunge) kwa mujibu wa katiba na pia haina ulazima wowote wa kutekelezwa. Lakini nakala ya hati hiyo tayari imetumwa kwa Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu yaani bunge la Iran.
-
Rouhani: Ni zamu ya kundi la 5+1 kutekeleza wajibu wake mkabala wa Iran
Apr 01, 2021 07:10Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu imetekeleza barabara wajibu wake na kufungamana na ahadi zake katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, na hivi sasa ni zamu ya kundi la 5+1 kutekeleza jukumu lake.