Sheikh Shahriyari: Waislamu wafanye juhudi za kusambaratisha siasa za kuwafarakanisha
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i68640-sheikh_shahriyari_waislamu_wafanye_juhudi_za_kusambaratisha_siasa_za_kuwafarakanisha
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu amesema kuwa, hii leo Ulimwengu wa Kiislamu unahitajia kuliko wakati mwingine wowote juhudi za kuondoa mapengo na mifarakano inayopandikizwa na maadui.
(last modified 2026-05-20T03:07:53+00:00 )
Apr 03, 2021 22:36 UTC
  • Sheikh Shahriyari: Waislamu wafanye juhudi za kusambaratisha siasa za kuwafarakanisha

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu amesema kuwa, hii leo Ulimwengu wa Kiislamu unahitajia kuliko wakati mwingine wowote juhudi za kuondoa mapengo na mifarakano inayopandikizwa na maadui.

Hujjatul Islam Sheikh Hamid Shahriyari amesema hayo akiwa huko Beirut mji mkuu wa Lebanon katika kumbukumbu ya Sheikh Ahmad Zein na kusisitiza kwamba, kuna haja kwa Waislamu kuongeza juhudi maradufu kwa ajili ya kuzisambaratisha njama za maadui zenye lengo la kuleta ugomvi na mifarakano katika Umma wa Kiislamu.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu madola ya kibeberu yakipata msaada wa vibaraka wao katika eneo la Asia Magharibi yamekuwa wakizusha vurugu, machafuko, migogoro ya kiuchumi na kiusalama na mapigano katika nchi za Kiislamu.

Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu

 

Aidha amesema lengo la njama hizo ni kuyadhoofisha mataifa yanayounga mkono muqawama na mapambano na kuleta ombwe katika serikali na tawala au kuunda serikali dhaifu ambazo hazitakuwa na taathira.

Katika upande mwingine Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu amekutana na kufanya mazungumzo na Sheikh Abdullah al Jabri Katibu Mkuu wa Harakati ya Umma ya Lebanon, ambapo wawili hao wamesisitiza  kuhusu umuhimu wa utoaji elimu katika maendeleo ya Umma wa Kiislamu na udharura wa kueneza na kusambaza elimu hiyo kwa ajili ya kupambana na ujinga; na kuongeza maarifa na uelewa wa elimu mbalimbali ili kukitaalamisha kizazi kijacho na kujenga ustaarabu wa kiutu.