Msimamo wa Iran kuhusu taarifa ya pamoja ya JCPOA
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i68624-msimamo_wa_iran_kuhusu_taarifa_ya_pamoja_ya_jcpoa
Jamhuri ya Kiislamu haitakubali mpango wowote wa kuondolewa vikwazo vikwazo vya Marekani hatua kwa hatua.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 03, 2021 05:35 UTC
  • Msimamo wa Iran kuhusu taarifa ya pamoja ya JCPOA

Jamhuri ya Kiislamu haitakubali mpango wowote wa kuondolewa vikwazo vikwazo vya Marekani hatua kwa hatua.

Hayo yamesemwa na maafisa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wakijibu taarifa ya Kamisheni ya Pamoja ya nchi wanachama wa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA. 

Kikako cha 17 cha Kamisheni ya Pamoja ya JCPOA kulifanya jana Ijumaa Aprili Pili kwa njia ya intaneti kikiwashirikisha wawakjilishi wa nchi za China, Ufaransa, Ujerumani, Russia, Uingereza na Iran. Mwishoni mwa kikao hicho kumetolewa taarifa iliyosisitiza kwamba, wanachama wa JCPOA wako tayari kujadili maudhui ya kurejea kikamilifi Marekani katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.

Akizungumzia suala hilo, afisa mmoja wa ngazi za juu wa Iran ameashiria sisitizo la Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Ali Khamenei katika hotuba yake ya tarehe 8 Januari aliposema kuwa: Jamhuri ya Kiislamu haitatekeleza majukumu yake katika fremu ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ila baada ya kuondolewa vikwazo vyote vya Marekani na kujihakikishia kwamba jambo hilo limefanyika kweli. Afisa huyo amesema matokeo yoyote ya Kamisheni ya Pamoja ya JCPOA ambayo yatatolewa kwa msingi wa kuondolewa vikwazo hivyo hatua kwa hatua au kufanyika mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Marekani, hayatakubalika. 

Wakati huo huo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Sayyid Abbas Araqchi ambaye ndiye aliyeongoza ujumbe wa Jamhuri ya Kiislamu katika kikao hicho, amesema suala la kurejea Marekani katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA halihitaji mazungumzo ya aina yoyote, na njia ya Washington katika kadhia hiyo iko wazi kabisa. Araqchi amesema: "Kama ilivyojiondoa katika makubaliano hayo na kuweka vikwazo haramu dhidi ya Iran, Marekani inaweza pia kurejea katika mapatano hayo na kukomesha ukiukaji wa sheria." 

Sayyid Abbas Araqchi

Msimamo na jibu hilo la Iran kuhusiana na taarifa ya Kamisheni ya Pamoja ya JCPOA lina nukta mbili muhimu:

Kwanza ni sisitizo la wazi la kuhuishwa haki za Iran katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA mkabala wa ukiukaji wa mapatano hayo wa Marekani. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, JCPOA ni mapatano ya pande kadhaa ya kimataifa yaliyoidhinishwa na azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Pili ni sisitizo la Iran la kuwepo utatuzi wa kimantiki wa kuondoka katika mkwamo wa sasa.

Mkuu wa Shirika la Atomiki la Iran, Ali Akbar Salehi alisema Ijumaa ya jana kwamba, mkwamo uliopo katika makubaliano ya JCPOA umo katika hali ya kuotoweka.

Hata hivyo swali lililopo hivi sasa ni kwamba, je, Marekani iko tayari kutupilia mbali sera na siasa zake zilizofeli za vikwazo na mashinikizo ya kiwango cha juu?

Marekani ilijiondoa kwa upande mmoja katika makubaliano hayo ya nyuklia na kurejesha vikwazo vilivyokuwa vimefutwa. Washington haikuishia hapo, bali iliiwekea Iran vikwazo vipya kwa visingizio bandia na vya uongo na ikazishinikiza nchi nyingine zitekeleze vikwazo hivyo.

Baada ya hatua hiyo ya Marekani, Jamhuri ya Kiislamu iliamua kupunguza utekelezaji wa baadhi ya vipengee vya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kwa mujibu wa vifungu nambari 26 na 36 za makubaliano hayo. Vifungu hivyo vinasema, iwapo upande wa pili hautatekeleza majukumu yake, Iran pia itakuwa na haki ya kusitisha utekeleza wa baadhi ya vipengee vya makubaliano hayo. Kwa nsingi huo Marekani haina njia nyingine ghairi ya kurejea katika njia ile ile iliyotumia kwa makosa kujiondoa katika makubaliano hayo. Hata hivyo inaonekana kuwa, nukta muhimu zaidi kwa sasa ni namna ya kurejea katika njia hiyo.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei anasisitiza kuwa: Iran itatekeleza vipengee vyote vya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA baada ya Marekani kufuta vikwazo vyake vyote kivitendo na si kwenye karatasi au kwa maneno matupu, na hatua hiyo ifanyiwe utafiti na Iran ili kuhakikisha kwamba imetekezwa kivitendo.