-
UN: Israel imeshaua Wapalestina wasiopungua 1,760 Ghaza wanaokimbilia msaada wa chakula
Aug 16, 2025 03:09Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imetangaza kuwa tangu mwishoni mwa mwezi Mei hadi sasa, jeshi la Israel limeshawaua Wapalestina wasiopungua 1,760 walipokuwa wakihangaika kupata msaada wa chakula huko Ukanda wa Ghaza likiwa ni ongezeko la mamia kadhaa tangu ilipotoa takwimu zake za mwisho mwanzoni mwa mwezi huu wa Agosti.
-
Mawaziri maluuni wa kizayuni wanaweza kupandishwa kizimbani ICC katika kesi ya kwanza ya apatheidi
Aug 16, 2025 02:30Maombi ya kutolewa waranti wa kuwatia nguvuni mawaziri wawili wa utawala wa kizayuni Israel wenye msimamo mikali ya chuki Itamar Ben-Gvir na Bezalel Smotrich kwa mashtaka ya kuhusika na ubaguzi wa rangi wa utenganishaji (apartheid) yamekamilika, lakini bado hayajawasilishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), kwa hofu ya vikwazo vya Marekani na mashinikizo kutoka nje.
-
Idadi ya wanaokufa kwa lisheduni Gaza inazidi kuongezeka
Aug 15, 2025 22:51Idadi ya watu wanaokufa kwa lisheduni katika Ukanda wa Gaza huko Gaza inazidi kuongezeka.
-
Sheikh Naim Qassim: Kamwe muqawama hautasalimisha silaha zake
Aug 15, 2025 07:47Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa , kamwe Kamwe muqawama hautasalimisha silaha zake.
-
HAMAS: Mpango wa Netanyahu wa 'Israel Kubwa Zaidi' ni tishio la wazi kwa mataifa ya Kiarabu na Waislamu
Aug 15, 2025 04:00Kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina HAMAS ametahadharisha kuhusu kupanuliwa kwa mipango ya ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kueleza kwamba hatua hiyo inakwenda sambamba na matamshi na ndoto za Benjamin Netanyahu kuhusu kuasisi "Israel Kubwa Zaidi."
-
Anas al-Sharif alimwambia mama yake ataondoka Ghaza ikiwa tu ni kwa ajili ya kuelekea Peponi
Aug 15, 2025 03:49Mama wa ripota Mpalaestina wa chaneli ya Aljazeera aliyeuliwa shahidi na jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel amesema, mwanawe alikataa katakata kuondoka Ukanda wa Ghaza akisisitiza kuwa atafanya hivyo ikiwa tu ni kwa ajili ya kuelekea Peponi.
-
Saudia, Misri, Qatar, Jordan, Kuwait, Iraq na Arab League zalaani kauli ya Netanyahu ya 'Israel Kubwa Zaidi'
Aug 14, 2025 23:05Nchi kadhaa za Kiarabu ikiwa na pamoja ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu zimetoa taarifa tofauti za kulaani matamshi ya waziri mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu ya kuunga mkono uwepo wa 'Israel Kubwa Zaidi' inayojumuisha maeneo ya kijiografia ya nchi kadhaa za Kiarabu.
-
Harakati ya Al-Nujabaa ya Iraq yatoa onyo kwa Marekani, Uingereza na utawala wa Kizayuni
Aug 14, 2025 23:00Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Iraq ya Al-Nujabaa amezionya Marekani, Uingereza na utawala wa Kizayuni wa Israel akisisitiza kuwa Muqawama wa Iraq umejiweka kwenye hali ya tahadhari.
-
Netanyahu aunga mkono kuwepo 'Israel Kubwa Zaidi' inayojumuisha Misri, Jordan, Syria na Lebanon
Aug 14, 2025 10:26Benjamin Netanyahu, waziri mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel ametamka kinagaubaga kuwa anatekeleza misheni ya kihistoria na ya kiroho ya kufikia lengo la kuwa na 'Israel Kubwa Zaidi' (Greater Israel) inayojumuisha maeneo ya kijiografia ya nchi kadhaa za Kiarabu zikiwemo Jordan, Misri, Syria, Lebanon, Iraq na Saudi Arabia.
-
Kwa muda wa siku 3, jeshi la kizayuni limebomoa nyumba 300 katika eneo la Zeitoun, Ghaza
Aug 14, 2025 09:37Jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel limebomoa zaidi ya nyumba 300 katika muda wa siku tatu zilizopita katika kitongoji cha Zeitoun katikati mwa Ukanda wa Ghaza ikiwa ni sehemu ya mpango wake linaouendeleza wa kulikalia kwa mabavu eneo hilo la ardhi ya Palestina.