Tahadhari kuhusu joto na ukosefu wa maji ya kunywa Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i128260
Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada kwa Ajili ya Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limetahadharisha kuhusu hali mbaya ya kiafya huko Gaza Palestina kutokana na ukosefu wa maji ya kunywa na usafi wa mazingira na matokeo ya joto.
(last modified 2025-07-13T03:31:01+00:00 )
Jul 13, 2025 03:31 UTC
  • Tahadhari kuhusu joto na ukosefu wa maji ya kunywa Gaza

Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada kwa Ajili ya Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limetahadharisha kuhusu hali mbaya ya kiafya huko Gaza Palestina kutokana na ukosefu wa maji ya kunywa na usafi wa mazingira na matokeo ya joto.

Shirika la UNRWA limebainisha kuwa, ukosefu wa maji ya kunywa na usafi wa mazingira huko Gaza, pamoja na msongamano wa watu katika makazi na joto la kiangazi, kutasababisha madhara makubwa ya kiafya.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada kwa Ajili ya Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limesisitiza kuwa, mzingiro dhidi ya Ukanda wa Gaza lazima uondolewe na turuhusiwe kuanza tena kutuma misaada ya kibinadamu huko Gaza, ikiwa ni pamoja na vifaa vya afya na usafi.

UNRWA imetahadharisha kwa mara nyingine tena kuhusu hali ya mgogoro wa binadamu katika Ukanda wa Gaza na uhaba mkubwa bidhaa za chakula. 

Wakati huo huuo, Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imeonya kwamba, mfumo wa chakula wa Gaza uko kwenye ukingo wa kuporomoka kabisa, huku hatua ya kuzuiwa msaada wa kibinadamu kuingia katika eneo hilo kukitishia maisha zaidi.

Huku viwango vya utapiamlo vinavyoongezeka maradufu miongoni mwa watoto na ugavi wa maziwa ya watoto wachanga ukipungua kwa kiwangi cha kutisha, mzozo wa kibinadamu huko Gaza unazidi kuongezeka, na kuweka maelfu ya maisha hatarini.