-
Duru ya kwanza ya mazungumzo ya kusitisha vita Kati ya Hamas, Israel yagonga mwamba
Jul 07, 2025 04:03Duru ya kwanza ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja ya kusitisha mapigano kati ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas na utawala wa Kizayuni wa Israel, iliyofanyika nchini Qatar, imemalizika bila mafanikio yoyote, kwa mujibu wa vyanzo viwili vya Palestina vinavyofahamu majadiliano hayo.
-
Jeshi la Yemen lajibu mapigo kwa kushambulia maeneo kadhaa ya Israel
Jul 07, 2025 02:49Jeshi la Yemen limefanya mashambulizi mapya ya makombora katika maeneo mbali mbali ya Israel katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, ili kulipiza kisasi cha mashambulizi ya anga ya utawala huo pandikizi dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Israel yaharakisha kuifanya kaskazini ya Ghaza ibaki bila wakazi kabla vita kusimamishwa
Jul 06, 2025 16:04Duru za kuaminika za Palestina zimeripoti kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unaharakisha kuhawamisha wakazi wa kaskazini ya Ghaza ili eneo hilo libaki tupu kabla ya kusimamishwa vita endapo mwafaka utafikiwa.
-
Ansarullah: Katika Uislamu wa Imamu Hussein (AS), kujisalimisha hakuna nafasi
Jul 06, 2025 15:03Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema, katika Uislamu wa Imamu Hussein (AS), kujidhalilisha na kusalimu amri hakuna nafasi hata chembe.
-
Sheikh Naim Qassem: Chaguo letu ni njia ya Imam Hussein, si udhalilifu na kusalimu amri
Jul 06, 2025 11:47Katibu Mkuu wa Hizbullah Sheikh Naim Qassem ametangaza kuwa, watu wa Lebanon kamwe hawatakubali kudhalilishwa au kusalimu amri mbele ya adui mzayuni, na kwamba njia yao itaendelea kubaki kuwa ya Imam Hussein iliyokita mizizi katika heshima, kutokubali kudhalilishwa na kujitolea muhanga.
-
Ben Gurion yafungwa tena kutokana na shambulio la kombora la Yemen
Jul 06, 2025 10:57Mamlaka ya anga ya Israel imesitisha safari zote za ndege za kuwasili na kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ben Gurion na kusema kuwa kituo hicho kitaendelea kufungwa "kwa muda usiojulikana" baada ya Vikosi vya Wanajeshi wa Yemen kufanya shambulio la kombora, kulipiza kisasi vita vya mauaji ya halaiki vinavyoendelea vya utawala wa Tel Aviv dhidi ya Wapalestina huko Gaza.
-
Sababu za Marekani na Israel kuwapiga risasi Wapalestina kwenye safu za misaada huko Gaza
Jul 05, 2025 22:55Wakandarasi wa usalama wa Marekani wanatumia risasi za moto, maguruneti, na gesi ya kuwasha dhidi ya raia katika vituo vya usambazaji wa misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza.
-
Israel yaua shahidi Wapalestina 64 katika Ukanda wa Gaza
Jul 05, 2025 11:55Mashambulizi ya Israel yamesababisha kuuawa shahidi Wapalestina 64 katika maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza tangu alfajiri ya leo Jumamosi, huku makumi ya waliouawa wakitambuliwa kama waombaji misaada, kwa mujibu wa ripoti kutoka hospitali za eneo hilo lililozingirwa.
-
Hamas yaonya, Msikiti wa al-Aqsa ni mstari mwekundu wa Muqawama
Jul 05, 2025 11:55Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas imeonya kuwa, Msikiti wa al-Aqsa ni "mstari mwekundu," na kuahidi kulinda eneo hilo takatifu dhidi ya mashambulizi ya mara kwa mara ya utawala wa Israel na uvamizi wa walowezi wa Kizayuni.
-
Hizbullah: Muqawama nchini Lebanon kamwe hautasalimu amri
Jul 05, 2025 11:52Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sheikh Naim Qassem amepinga mwito wa serikali ya Beirut wa kuweka chini silaha kundi hilo la Muqawama na kusema kuwa, "sisi si watu wa kusalimu amri."