Ansarullah: Katika Uislamu wa Imamu Hussein (AS), kujisalimisha hakuna nafasi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i128018
Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema, katika Uislamu wa Imamu Hussein (AS), kujidhalilisha na kusalimu amri hakuna nafasi hata chembe.
(last modified 2025-07-10T12:29:42+00:00 )
Jul 06, 2025 18:33 UTC
  • Ansarullah: Katika Uislamu wa Imamu Hussein (AS), kujisalimisha hakuna nafasi

Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema, katika Uislamu wa Imamu Hussein (AS), kujidhalilisha na kusalimu amri hakuna nafasi hata chembe.

Abdul-Malik Badruddin al-Houthi, Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah alisema hayo jana wakati akitoa hotuba kwenye matembezi na marasimu ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hussein AS, katika mji mkuu wa Yemen, Sana'a,

Akihutubia umati mkubwa uliohudhuria kumbukumbu hiyo, Badruddin al-Houthi ameeleza bayana kuwa, "Uislamu ambao Imam Hussein AS aliuawa shahidi kwayo ni Uislamu unaohimiza amani na wala sio kujisalimisha."

"Uhalifu unaofanywa leo na maadui dhidi ya umma wa Kiislamu, unafanya kuwa maradufu wajibu wetu wa kidini kukabiliana na dhulma za Marekani na Israel."

Abdul-Malik Badruddin al-Houthi, Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah amesema, "Kujisalimisha mkabala wa jinai na ufisadi wa Marekani na Israel hakutakuwa na matokeo mengine ghairi hasara na fedheha."

Amebainisha kuwa, "Leo tunashuhudia kukua na kupanuka kwa vuguvugu la Muqawama katika Umma wa Kiislamu, unapokabiliana na ukandamizaji wa Marekani na Israel huko Gaza, Lebanon, Iran, Iraq na Yemen."

Ameongeza kuwa, "Mpango wa Kizayuni ni wa kichokozi na wa uharibifu, na unalenga taifa la Kiislamu, na kamwe hatutasita kusimama dhidi yake."