-
Msimamo mmoja wa nchi za Kiislamu na Kiarabu katika kulaani jinai za Israel dhidi ya Gaza
Nov 13, 2024 23:09Kikao cha dharura cha viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kwa ajili ya kuunga mkono kadhia ya Palestina kilifanyika siku ya Jumatatu mjini Riyadh Saudi Arabia, ambapo msimamo wa pamoja unaolaani jinai za kinyama za utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Palestina Lebanon ulipitishwa katika taarifa ya mwisho ya kikao hicho.
-
Kwa mara ya kwanza Hizbullah yakishambulia kituo kikubwa cha jeshi la anga la Israel
Nov 13, 2024 08:32Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Lebanon, Hizbullah, kwa mara ya kwanza, imeshambulia kwa makombora kambi kubwa ya jeshi la anga la utawala wa Kizayuni wa Israel, ikiwa ni sehemu ya ulipizaji kisasi dhidi ya ukatili unaofanywa na utawala huo ghasibu.
-
Umoja wa Mataifa: Israel ilikwamisha asilimia 85 ya majaribio ya kupelekwa misaada Gaza
Nov 13, 2024 03:38Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, asilimia 85 ya majaribio yake ya kuratibu misafara ya misaada na ziara za kibinadamu kaskazini mwa Gaza yalikataliwa au kuzuiwa na mamlaka ya Israel mwezi uliopita.
-
Netanyahu ajificha kwenye 'chumba cha chini ya ardhi' kwa kuhofia mapigo ya Wanamuqawama
Nov 12, 2024 22:48Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ameripotiwa kuwa anafanya kazi kutoka kwenye "chumba cha chini ya ardhi" kwa hofu ya ulipizaji kisasi na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani na harakati za Muqawama wa Kiislamu katika eneo la Asia Magharibi.
-
Maafisa watano wa jeshi la Israel waangamizwa kaskazini mwa Ghaza
Nov 12, 2024 09:16Maafisa wengine watano wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel wameangamizwa na wanamapambano wa Kiislamu kaskazini mwa Ukanda wa Ghaza katika kipindi cha saa 24 zilizopita.
-
Taarifa ya kikao cha Riyadh yasisitiza kuliunga mkono kwa dhati taifa la Palestina
Nov 12, 2024 04:22Washiriki wa kikao cha viongozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu kilichofanyika mjini Riyadh, Saudi Arabia wamesisitiza umuhimu wa kuzingatiwa suala la Palestina kama kadhia kuu na kuwaunga mkono kwa dhati wananchi wa taifa hilo ili wapate haki zao za kitaifa na zenye uhalali.
-
Jeshi la Israel laua Wapalestina 14 Ghaza baada ya kuua Walebanon 14 pia Bekaa
Nov 12, 2024 04:21Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limeendelea kufanya jinai za mauaji ya kinyama katika Ukanda wa Ghaza kwa kuwaua shahidi Wapalestina 14 asubuhi ya leo waliokuwa wamepata hifadhi katika linalodaiwa na utawala huo kuwa ni "eneo salama" huko al-Mawasi.
-
Jihadul Islami: Maneno ya waziri wa fedha wa Israel yamewazaba kibao wafanya mapatano
Nov 12, 2024 04:20Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina imetangaza katika taarifa kwamba, kauli ya Waziri wa Fedha wa utawala wa Kizayuni kuhusu kuukalia kwa mabavu Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan imewazaba kibao kingine wafanya mapatano.
-
Muqawama wa Kiislamu wa Iraq washambulia ngome na vituo vya utawala wa Kizayuni
Nov 12, 2024 03:39Muqawama wa Kiislamu wa Iraq umetangaza kuwa umefanya shambulizi la ndege isiyo na rubani kwenye kituo cha kijeshi kusini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu zilizopewa jina bandia la Israel.
-
Viongozi wa Kiislamu wataka kukomeshwa mara moja jinai za Israel huko Ghaza na Lebanon
Nov 12, 2024 00:24Viongozi wa Kiislamu na wa Kiarabu ambao wameitisha mkutano wa dharura mjini Riyadh Saudi Arabia wameutaka utawala wa Kizayuni ukomeshe mara moja jinai zake za kinyama katika Ukanda wa Ghaza na Lebanon.