-
Kwa nini Trump amemwekea vikwazo Rais wa Cuba?
Jul 13, 2025 10:30Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imetangaza vikwazo vipya vya fedha dhidi ya Rais wa Cuba Miguel Díaz-Canel na maafisa wengine waandamizi wa nchi hiyo pamoja na marufuku ya usafiri kwa kisingizio cha kukandamiza maandamano ya amani yaliyofanyika mwaka 2021.
-
Mashabiki wa Glasgow Rangers wampinga mshambuliaji Muisraeli kuingia timu hiyo kutokana na mauaji ya kimbari Gaza
Jul 13, 2025 10:11Mashabiki wa Klabu ya Soka ya Glasgow Rangers huko Uskochi, Uingereza, wameanzisha kampeni kubwa ya kuzuia kusajiliwa kwa mshambuliaji kutoka Israel, kama njia ya kupinga vita vya muda mrefu vya mauaji ya kimbari vinavyotekelezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya raia wa Palestina wanaoishi Ukanda wa Gaza unaozingirwa.
-
Jibu la suali la leo; kwa nini Albanese anasema hakuna tena mistari myekundu baada ya yeye kuwekewa vikwazo na Marekani?
Jul 13, 2025 04:28Francesca Albanese, Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu, ametangaza kwamba uamuzi wa Marekani wa kumuwekea vikwazo unaonyesha kuwa hakuna tena mstari mwekundu wowote.
-
Polisi UK yakamata makumi ya watu kwa kushiriki maandamano ya kuiunga mkono Palestina
Jul 13, 2025 03:36Polisi wa Uingereza imewakamata makumi ya wanaharakati wanaoiunga mkono Palestina wakati wa maandamano mapya ya kupinga marufuku ya vuguvugu la 'Palestine Action', kundi linalojulikana kwa maandamano yake dhidi ya makampuni ya silaha yenye uhusiano na Israel.
-
Trump ashadidisha vita vya kibiashara dhidi ya Mexico, EU
Jul 13, 2025 02:34Rais Donald Trump wa Marekani ametishia kuziwekea bidhaa zinazoingia nchini humo kutoka Mexico na Umoja wa Ulaya ushuru wa asilimia 30 kuanzia Agosti Mosi.
-
Russia yaonya US, waitifaki: Msiitishie Russia na Korea Kaskazini
Jul 12, 2025 13:15Moscow imeionya Marekani na waitifaki wake dhidi ya kuzitishia Russia na Korea Kaskazini.
-
Wabunge 60 wa UK waitaka London ilitambue taifa la Palestina
Jul 12, 2025 12:50Kufuatia mpango tata wa Israel wa kuwahamisha kwa nguvu wakazi wa Gaza na kuwapeleka Rafah, takriban wabunge 60 wa Uingereza wameitaka serikali ya London kulitambua rasmi taifa la Palestina.
-
Mabadiliko ya tabianchi; vimbunga vya vumbi vimeathiri watu milioni 330 duniani
Jul 12, 2025 10:39Ripoti mpya ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) imebainisha kuwa, dhoruba za mchanga na vumbi zinaongoza kwa "vifo vya mapema" kutokana na mabadiliko ya tabianchi, ambapo zaidi ya watu milioni 330 katika nchi 150 wameathirika.
-
UNESCO: Mauaji ya wanasayansi wa Iran ni pigo kwa jumuiya ya sayansi duniani
Jul 12, 2025 10:18Katibu Mkuu wa Kamisheni ya Kitaifa ya Iran ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Hassan Fartousi, amesema hujuma za Israel dhidi ya Iran ni tishio kwa "mantiki, sayansi na amani."
-
Pentagon yakiri: Kombora la Iran lilitwanga kambi ya US ya Al-Udeid, Qatar
Jul 12, 2025 08:56Katika pigo kubwa kwa heshima ya kijeshi ya Marekani, Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo (Pentagon) imekiri kwamba, moja ya makombora ya balestiki ya Iran ilipiga moja kwa moja kambi ya anga ya jeshi la US la Al-Udeid nchini Qatar, wakati wa shambulio la kulipiza kisasi la Tehran mwezi uliopita.