-
Upanga wa China uko juu ya viwanda vya kijeshi vya Magharibi
Jun 10, 2025 04:10Vikwazo ambayo China imeziwekea nchi za Ulaya na Marekani katika usafirishaji wa madini adimu na sumaku zinazotengenezwa kutokana na madini hayo, vimeleta changamoto kubwa kwa shughuli za kijeshi za Marekani na washirika wake wa Ulaya.
-
Siasa za kupinga uhamiaji huko Los Angeles zaibua mvutano kati ya serikali ya shirikisho na za majimbo?
Jun 09, 2025 06:43Hitilafu kuhusu siasa za kupinga uhamiaji na jinsi ya kukabiliana na waandamanaji huko Los Angeles zimeibua mvutano mkali kati ya serikali ya shirikisho ya Marekani na serikali ya Jimbo la California.
-
Polisi Marekani watumia risasi kuwatawanya waandamanaji Los Angeles
Jun 09, 2025 03:28Maafisa wa usalama nchini Marekani wametumia gesi ya kutoa machozi na risasi za plastiki katika mji wa Los Angeles siku ya Jumapili, kufuatia hatua ya Rais Donald Trump kupeleka jeshi linalojulikana kama Gadi ya Kitaifa kwa ajili ya kukandamiza maandamano yaliyozuka kupinga dhulma dhidi wahamiaji.
-
Mgombea urais Colombia apigwa risasi kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi
Jun 08, 2025 09:02Mgombea urais wa Colombia amepigwa risasi tatu wakati akiwa katika hafla ya kampeni katika mji mkuu, Bogota. Miguel Uribe Turbay, (39), alishambuliwa alipokuwa akihutubia umati mdogo katika bustani siku ya Jumamosi.
-
Kwa nini Marekani imewawekea vikwazo majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai?
Jun 08, 2025 03:15Marekani mnamo Alhamisi, Juni 5, iliwawekea vikwazo majaji wanne wa kike wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai kwa kushughulikia kesi zinazohusiana na Israel na hatua za Marekani nchini Afghanistan. Vikwazo hivyo, ambavyo mara nyingi huwekewa maafisa kutoka nchi zinazopinga Marekani, sasa vimewalenga maafisa wa mahakama ya kimataifa.
-
Ufaransa yasisitiza kuhusu azma ya kutambua taifa la Palestina
Jun 07, 2025 09:28Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Noël Barrot, amesema kuwa Paris bado imejizatiti kutambua rasmi taifa la Palestina katika mkutano wa Umoja wa Mataifa unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.
-
UN yakemea vikali vikwazo vya Marekani dhidi ya majaji wa ICC
Jun 07, 2025 09:07Volker Türk Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, amelaani uamuzi wa hivi karibuni wa serikali ya Marekani wa kuweka vikwazo dhidi ya majaji wanne wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), akisema kuwa hatua hiyo inahatarisha misingi ya utawala bora na usimamizi huru wa haki.
-
UN: Tumesikitishwa mno na vikwazo vya US dhidi ya majaji wa ICC
Jun 07, 2025 03:29Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk amesema "amesikitishwa sana" na vikwazo vya serikali ya Marekani dhidi ya majaji wanne wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).
-
Wafanyakazi wa bandari Ufaransa, Italia wazuia kupelekwa silaha Israel
Jun 07, 2025 03:28Wafanyakazi wa bandari za Ufaransa na Italia wameendelea kufanya mgomo wao na kukataa kupakia shehena za silaha na zana za kijeshi zinazopelekwa Israel, wakisema kuwa hawatahusika katika "mauaji ya halaiki" yanayoendelea Gaza.
-
Chuo cha Trinity Ireland chakata uhusiano na Isreal kulalamikia mauaji ya Gaza
Jun 06, 2025 23:02Chuo Kikuu cha Trinity cha Iralend kimekata uhusiano wake na utawala haramu wa Israel kama hatua ya kulalamikia jinai zinazofanywa na utawala huo dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza huko Palestina.