-
Mkaguzi mkuu wa magereza Ufaransa: Hali ya magereza nchini ni "mbaya, ya aibu na ya majanga"
Jun 01, 2026 02:39Wizara ya Sheria ya Ufaransa imetangaza kwamba idadi ya wafungwa nchini humo imefikia zaidi ya watu 88,600, ambayo ni kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa katika historia ya nchi hiyo.
-
Umoja wa Wanazuoni Waislamu: Kuanzisha uhusiano na Israel kuna madhara kwa nchi za Kiislamu
May 31, 2026 12:52Umoja wa Wasomi wa Kiislamu Duniani umetangaza upinzani wake kamili kwa tishio lolote linaloelekezwa kwa nchi za Kiislamu au mataifa yao kutoka upande wowote ule, na kuonya kuhusu matokeo mabaya ya kunzisha uhusiano na utawala wa Tel Aviv.
-
Simulizi la Wall Street Journal kuhusu vita vya Marekani dhidi ya Iran: Ni ushindi wa kimaonyesho wa Trump au kushindwa halisi?
May 31, 2026 12:50Mhariri mkuu wa Wall Street Journal amesema: "Trump analazimika kudhihirisha kushindwa kwake mbele ya Iran kama ushindi ili kulinda sura na hadhi yake."
-
Utafiti: Wamarekani wengi wanasumbuliwa na njaa kuliko wakati wa janga la Covid-19
May 31, 2026 04:22Utafiti wa Benki ya Hifadhi ya Shirikisho ya New York unaonyesha kwamba karibu 10% ya kaya zinaripoti kutokula chakula kutokana na kupanda kwa gharama na matatizo ya kifedha.
-
Kwa nini makubaliano yoyote na Iran ni fedheha kwa Trump?
May 29, 2026 12:41Kadiri uwezekano wa kufikiwa makubaliano kati ya Marekani na Iran unavyoongezeka, waandishi wa habari na wachambuzi mashuhuri wa Marekani wanatoa maoni yao kwa uwazi zaidi kuhusu kushindwa Trump na Netanyahu kutimiza matakwa yao katika mashambulio ya kijeshi dhidi ya Iran.
-
CNN: Trump amezitishia au kuzishambulia nchi 15 akiwa madarakani
May 29, 2026 03:05Ripoti ya televisheni ya CNN imeeleza kuwa Rais Donald Trump wa Marekani amezitishia, ameeleza wazi uwezekano wa kufanya mashambulizi au amezishambulia nchi 15 katika mihula yake miwili ya uongozi; yaani kwa mahesabu ya haraka amefanya hivyo kwa nchi moja kati ya kila nchi 13 duniani.
-
Marekani yarejesha vikwazo dhidi ya Ripota Maalumu wa UN kwa kufichua mauaji ya kimbari ya Israel
May 28, 2026 10:40Marekani imemuwekea tena vikwazo Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu kwa sababu tu ya kufichua mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
-
Russia yaunga mkono msukumo wa Afrika wa kudai fidia kutoka kwa madola ya kikoloni
May 27, 2026 03:06Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergey Lavrov, amesema nchi yake inaunga mkono msukumo wa Afrika wa kutaka fidia kutoka kwa madola ya kikoloni. Akizungumza katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Afrika mjini Moscow, Lavrov amesema suala hilo ni sehemu ya mapambano mapana dhidi ya ukoloni mambo-leo.
-
Mahujaji wanasimama Arafa leo kutekeleza nguzo muhimu ya Hija
May 26, 2026 03:17Mamilioni ya Mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu, Al Kaaba, leo wanasimama katika uwanja wa Arafa katika kilele cha ibada tukufu ya Hija.
-
Papa Leo aomba radhi kutokana na nafasi ya Kanisa Katoliki katika biashara ya utumwa ya kuvuka Bahari ya Atlantiki
May 26, 2026 03:04Katika hatua ya kihistoria, Papa Leo wa XIV Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani ameomba radhi kutokana nafasi ya Baraza Kuu la Uongozi wa Kanisa Katoliki na Vatican la kuhalalisha utumwa na kushindwa kulaani suala hilo kwa karne kadhaa.