Aljazeera: Trump anatafuta njia ya kutoka vitani kwa heshima
-
Trump na Netanyahu
Mwandishi wa kituo cha Aljazeera huko Washington anasema kuwa Rais Donald Trump Marekani anatafuta jinsi ya kutoka kwenye vita na Iran kwa njia ya heshima.
Katika uchambuzi wake wa misimamo ya hivi karibuni ya Donald Trump, Rais wa Marekani, kuhusu Iran, Aljazeera imeandika kuwa: Trump anatafuta “njia ya kutoroka kwa heshima” kutoka katika mzozo wa sasa, lakini ujumbe wake haueleweki na unapingana kiasi kwamba haiwezekani kuelewa kama kweli kuna mazungumzo yoyote yanaendelea au la.
Kwa mujibu wa Pati Kalhein, mwandishi wa Aljazeera huko Washington, katika saa 24 zilizopita Trump amedai kwenye mitandao ya kijamii kwamba Iran “imekubali matakwa yote ya Marekani bila kupata chochote.” Kwa upande mwingine, Iran imefunga tena Lango Bahari la Hormuz.
Trump pia amesema kuwa mzingiro wa baharini wa Marekani unaendelea na kwamba meli 13 zimesimamishwa, ingawa ni vigumu sana kupatikana uthibitisho huru wa madai haya.”
Wakati Trump amedai mara kadhaa kwamba atamaliza vita na Iran “ndani ya siku chache” na leo pia ameahidi kutoa taarifa mpya, Alazeera imesisitiza kuwa: Hakuna taarifa yoyote kuhusu ni nani anaongea na nani, maudhui ya mazungumzo au hatua zinazofuata.
Mwandishi wa al Jazeera huko Washington anasema: Kwa sasa hakuna njia ya kujua kwamba kuna mazungumzo yanayofanyika baina ya Marekani na Iran.”