Wamarekani: Upungufu wa akili wa Trump umeongezeka
https://parstoday.ir/sw/news/world-i137858-wamarekani_upungufu_wa_akili_wa_trump_umeongezeka
Mshauri wa Mkuu wa zamani mkuu wa Ikulu ya White House wakati wa muhula wa kwanza wa Donald Trump ameonya kuwa upungufu wa akili wa rais wa Marekani umeongezeka kwa kiasi kikubwa.
(last modified 2026-04-19T10:50:31+00:00 )
Apr 19, 2026 10:39 UTC
  • Donald Trump
    Donald Trump

Mshauri wa Mkuu wa zamani mkuu wa Ikulu ya White House wakati wa muhula wa kwanza wa Donald Trump ameonya kuwa upungufu wa akili wa rais wa Marekani umeongezeka kwa kiasi kikubwa.

Ty Cobb, mshauri mkuu wa zamani wa Ikulu katika muhula wa kwanza wa Trump, amesema: “Rais wa Marekani amechanganyikiwa kabisa na yuko katika hali ya tahayuri. Msamiati wake umepungua, amekimbilia kwenye matusi na vitisho, anatenda bila kufikiri, na hii inaonyesha kuwa hana udhibiti wowote juu ya mienendo yake ya ghafla.”

Cobb ameongeza kuwa “upungufu wa uwezo wa kiakili wa Trump umekithiri kwa kasi zaidi kuliko wakati wa muhula wake wa kwanza.” Amesema pia: “Mojawapo ya dalili za kawaida za ugonjwa wa Alzheimers ni usumbufu katika mzunguko wa usingizi na kuamka. Tunaona maneno yake ya wazimu mtandaoni saa kumi alfajiri, na tunamshuhudia akisinzia katika mikutano ya baraza la mawaziri asubuhi na alasiri, hii ni ishara ya wazi ya ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu.”

Wakati huohuo, Tim Walz, gavana wa jimbo la Minnesota, naye amesema kuwa Trump ni mtu asiye na akili timamu, mwenye tabia hatari na asiyeweza kutabirika.

“Tunaye rais ambaye aliiingiza Marekani vitani bila tishio lolote halisi, bila malengo ya wazi, na bila mpango wowote wa kujiondoa vitani," mesema Tim Walz.