-
Baraza la Uhusiano wa Marekani na Uislamu lalaani uporaji vipaza sauti na marufuku ya adhana misikitini Palestina
Dec 04, 2024 23:32Baraza la Mahusiano Marekani na Uislamu limelaani kitendo cha kunyang'anywa vipaza sauti na kupigwa marufuku adhana misikitini katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na kuitaja hatua hiyo kuwa tangazo la wazi la vita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Uislamu.
-
Upinzani nchini Korea Kusini wataka Rais auzuliwe, umeapa kumfungulia mashtaka
Dec 04, 2024 09:21Chama kikuu cha upinzani nchini Korea Kusini kimetangaza - leo, Jumatano - kwamba kimewasilisha ombi la kumuondoa madarakani Rais Yoon Suk Yeol, baada ya kutangaza nia yake ya kumfungulia mashitaka pamoja na wasaidizi wake wakuu wa masuala ya usalama kwa tuhuma za "uasi," kufuatia hatua yake ya kutangaza sheria za kijeshi nchini, hatua ambayo ilizuiliwa haraka na Bunge.
-
Waziri wa Algeria atoka nje ya mkutano India kulalamikia kuwepo waziri wa utawala wa Kizayuni wa Israel
Dec 04, 2024 02:35Ujumbe wa Algeria, ukiongozwa na Waziri wake wa Biashara Tayeb Zitouni, umetuma salamu za kijasiri na za kivitendo katika Mkutano wa Ushirikiano (Patnership Summit) uliofanyika New Delhi, India kwa kutoka nje ya ukumbi mara baada ya kuwasili waziri wa uchumi wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Ripoti: Uchumi wa Iran ulistawi kwa 4% kuanzia Aprili hadi Septemba
Dec 03, 2024 23:57Kituo cha Takwimu cha Iran (SCI) kimeripoti upanuzi wa 4% katika uchumi wa Iran katika nusu ya kwanza ya mwaka wa kalenda ya Kiirani ulioanza Machi 21.
-
Mkutano wa UN kuhusu kuenea majangwa duniani umeanza Riyadh, Saudi Arabia
Dec 03, 2024 08:51Wazungumzaji katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa kupambana na kuenea majangwa duniani COP16 unaoendelea nchini Saudi Arabia wametahadharisha kuwa hatua zinapasa kuchukuliwa ili kulinda uhai duniani.
-
Mkuu wa ICC aikosoa Marekani kwa kuingilia utendaji wa mahakama hiyo
Dec 03, 2024 03:49Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ameikosoa Marekani kwa kuingilia uchunguzi wa taasisi hiyo na kuyataja mashambulizi dhidi ya mahakama hiyo kuwa ya kutisha.
-
Mashirika ya silaha ya Marekani yazidi kujitajirisha kwenye dimbwi la damu
Dec 02, 2024 23:20Takwimu za hivi karibuni kabisa zilizotolewa na taasisi ya amani ya Stockholm International Peace Research Institute (SIPRI) zinaonesha kuwa, mashirika yanayozalisha silaha duniani ambayo asilimia kubwa ni ya Marekani, yamepata faida kubwa kupindukia kwa kuuza silaha zilizoishia kumwaga damu za watu kwenye kona mbalimbali za dunia hasa barani Asia.
-
Vitisho vya Trump dhidi ya mataifa wanachama wa BRICS
Dec 02, 2024 23:19Donald Trump, rais mteule wa Marekani, amezitishia nchi wanachama wa kundi la BRICS kwamba ikiwa zitajaribu kuanzisha sarafu nyingine itakayokuwa mbadala wa dola ya Marekani, ataziwekea bidhaa zao ushuru wa kibiashara wa 100%.
-
Cuba: Tuko pamoja na wananchi na serikali ya Syria
Dec 02, 2024 09:11Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba ametangaza kuwa nchi hiyo inatangaza mshikamano wake na iko pamoja na wananchi na serikali ya Syria kufuatia kushtadi hujuma za karibuni za makundi ya kigaidi katika ardhi ya Syria.
-
White House yakiri kuhusu nafasi muhimu ya Hamas
Dec 02, 2024 08:28Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani amekiri kuhusu nafasi muhimu ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) katika eneo.