Cuba: Tuko pamoja na wananchi na serikali ya Syria
(last modified Mon, 02 Dec 2024 12:41:27 GMT )
Dec 02, 2024 12:41 UTC
  • Cuba: Tuko pamoja na wananchi na serikali ya Syria

Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba ametangaza kuwa nchi hiyo inatangaza mshikamano wake na iko pamoja na wananchi na serikali ya Syria kufuatia kushtadi hujuma za karibuni za makundi ya kigaidi katika ardhi ya Syria.

Bruno Rodriguez ametuma ujumbe katika mtandao wa kijamii wa X akibainisha uungaji mkono wa serikali ya Havana kwa Syria na kutaka kuheshimiwa mamlaka ya taifa na umoja wa ardhi yote ya nchi hiyo.  

Makundi ya kigaidi katika maeneo ya kaskazini na kaskazini magharibi mwa Syria yalishambulia kambi za jeshi la Syria katika viunga vya magharibi mwa mji wa Halab tangu Jumatano asubuhi tarehe 27 mwezi Novemba mwaka huu. 

Kufuatia hujuma hizo za magaidi, jeshi la Syria pia siku kadhaa zilizopita zilishambulia maeneo yanayoshikiliwa na magaidi nchini humo. 

Kamandi ya Jeshi la Syria ilitangaza katika taarifa yake siku ya Jumapili kuwa mchakato wa kukabiliana na mashambulizi ya kigaidi unaendelea kwa mafanikio na irada thabiti; na kwamba hivi karibuni litetekeleza mashambulizi ili kukomboa maeneo yote yanayoshikiliwa na magaidi.