Mkuu wa ICC aikosoa Marekani kwa kuingilia utendaji wa mahakama hiyo
Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ameikosoa Marekani kwa kuingilia uchunguzi wa taasisi hiyo na kuyataja mashambulizi dhidi ya mahakama hiyo kuwa ya kutisha.
Akizungumza katika mkutano wa kila mwaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), Jaji Tomoko Akane amesema: Mahakama hiyo inatishiwa kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na mwanachama mwingine wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (Marekani) kana kwamba ni shirika la kigaidi.
Jaji Akane ameashiria matamshi ya Seneta wa Marekani Lindsey Graham, ambaye aliita Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kuwa nii "mzaha wa hatari" na kuomba Bunge la Marekani limuwekee vikwazo mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo.
Awali Graham alisema katika mahojiano na gazeti la "Fox News" kwamba anahutubia washirika wa Marekani kama Canada, Uingereza, Ujerumani, na Ufaransa, kwamba iwapo wataisaidia Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC, basi Washington pia itawawekea vikwazo.
Hivii karibuni, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ilitoa hati ya kukamatwa Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel, Benjamin Netanyahu, na aliyekuwa waziri wake wa vita Yoav Gallant, wakituhumiwa kutenda jinai za vita.
Uamuzi huo umeikasirisha mno Marekani ambayo daima imekuwa ikiikingia kifua Israel inayotenda jinai dhidi ya binadamu na mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza.