-
Wabunge wa Democratic wamthibitishia Biden, Israel inakiuka sheria za Marekani
May 04, 2024 03:27Wabunge wa chama cha Democratic cha Marekani wamesema katika barua waliyomwandikia Rais Joe Biden wa nchi hiyo kwamba wanaamini kuna ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha kwamba Israel imekiuka sheria za Marekani kwa kuzuia mtiririko wa misaada ya kibinadamu kwa watu wa Ukanda wa Gaza unaoendelea kushambuliwa kinyama na jeshi la utawala wa Kizayuni.
-
Kremlin: Kauli za Macron kuhusu kutuma vikosi nchini Ukraine ni hatari sana
May 04, 2024 03:26Ofisi ya Rais wa Russia jana Ijumaa ilishutumu kauli zilizotolewa na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, kuhusu uwezekano wa Paris kuingia katika vita vya Ukraine, na kuzitaja kuwa ni "mwenendo hatari sana."
-
Mwendesha Mashtaka ICC akemea vitisho vya Marekani na Israel
May 04, 2024 03:25Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imetoa wito wa kusitishwa vitisho kwa wafanyakazi wa mahakama hiyo, ikisema kuwa vitisho hivyo vinaweza kuwa uhalifu dhidi ya mahakama hiyo inayoshughulikia uhalifu wa kivita.
-
Tuzo la Uhuru wa Vyombo vya Habari 2024 yatolewa kwa waandishi habari wa Gaza
May 03, 2024 23:44Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), limetoa tuzo yake ya mwaka kwa waandishi wa habari wa Gaza, kwa mnasaba wa Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani.
-
Kuongezeka ukatili dhidi ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Marekani wanaounga mkono Palestina
May 03, 2024 07:14Huku maandamano ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya Marekani yakiendelea kufanyika kwa lengo la kupinga jinai za utawala wa Kizayuni huko Gaza na vilevile kwa ajili ya kuwaunga mkono Wapalestina, polisi wa nchi hiyo wameongeza hatua zao za ukandamizaji dhidi ya wanafunzi hao.
-
Polisi wa Marekani watumia mabavu kuwatawanya wanafunzi wanaounga mkono Palestina
May 03, 2024 07:08Polisi wa kuzima ghasia nchini Marekani wameibomoa kambi ya wanafunzi wanaoandamana kwa amani kuunga mkono Palestina katika Chuo Kikuu cha California huko Los Angeles, siku moja baada ya wanafunzi hao kushambuliwa na wafuasi wanaounga mkono utawala haramu wa Israel.
-
Trump: Nikichaguliwa kuwa Rais nitarejesha marufuku ya Waislamu kuingia Marekani
May 03, 2024 04:16Donald Trump mgombea anayetarajiwa kuteuliwa na chama cha Republican kuwania kkiti cha urais nchini Marekani amesema kuwa, akichaguliwa atarejesha tena marufuku ya kusafiri kwa baadhi ya nchi zenye Waislamu wengi katika siku ya kwanza ya utawala wake mpya.
-
Waislamu wa US: Muswada wa Bunge wa marufuku ya hotuba dhidi ya Israel 'unakandamiza' uhuru wa kujieleza
May 03, 2024 00:31Jumuiya kubwa ya kutetea haki za kiraia za Waislamu nchini Marekani imelishutumu Baraza la Wawakilishi (Congress) kwa kuidhinisha muswada wenye utata unapiga marufuku ukosoaji wowote dhidi ya Israel.
-
Uingereza yaanza kuwashikilia wahamiaji wanaotarajiwa kupelekwa Rwanda
May 02, 2024 04:01Mamlaka husika nchini Uingereza zimeanza kuwashikilia wahamiaji kama sehemu ya maandalizi ya kuwahamishia nchini Rwanda katika muda wa wiki 9 hadi 11 zijazo. Serikali ya London ilitangaza taarifa hiyo jana ikiashiria hatua muhimu katika mkakati wa uhamiaji unaotekelezwa na Waziri Mkuu Rishi Sunak.
-
Polisi ya Ufaransa yakandamiza maandamano ya Siku ya Wafanyakazi Duniani mjini Paris
May 02, 2024 03:56Polisi wa kutuliza ghasia wa Ufaransa jana walikabiliana kwa mabavu na washiriki wa maandamano katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) katika mji mkuu wa nchi hiyo, Paris.