-
Waandishi wakosoaji wa Israel wasusia tamasha la jumuiya ya PEN America
Apr 23, 2024 06:54Tamasha ya Jumuiya ya Kalamu ya Marekani (PEN America) imefutwa kutokana na ukosoaji mkubwa wa waandishib walioalikwa katika sherehe hiyo dhidi ya jinai na uhalifu unaofanywa na Israel huko Gaza.
-
Onyo jipya kuhusu kuingia NATO katika vita vya Ukraine
Apr 23, 2024 00:55Viktor Orbán, Waziri Mkuu wa Hungary amesema katika taarifa kwamba viongozi wa Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Kujihami ya Kijeshi ya Magharibi (NATO) wanauchukulia mzozo wa Moscow na Kyiv kuwa ni wao na wala hawazingatii hatari ya kujihusisha na mzozo huo. Ameonya kuwa NATO inakaribia kutuma askari wake huko Ukraine.
-
Sunak: Safari za kwanza za ndege kuelekea Rwanda za wanaotafuta hifadhi zitaanza baada ya wiki 10 hadi 12
Apr 22, 2024 23:38Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak, ameahidi kwamba safari za kwanza za ndege za nchi hiyo za raia wa nchi mbalimbali wanaotafuta hifadhi zitaanza kuondoka Uingereza kuelekea Rwanda baada ya wiki 10-12.
-
Hamu ya Wamarekani kupiga kura imepungua kwa kiwango kisicho na mfano
Apr 22, 2024 02:48Uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa na Chaneli ya NBC News umeonyesha kuwa, Wamarekani wanapoteza hamu ya kupiga kura katika uchaguzi wa rais wa mwaka huu kwa sababu mgombea wa chama cha Democrat Joe Biden na mpinzani wake wa chama cha Republican Donald Trump, wote wawili hawana mvuto kwa wapiga kura.
-
Maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya Uislamu yafanyika mjini Paris
Apr 22, 2024 02:48Baada ya mabishano mengi na ruhusa iliyotolewa na mahakama ya kiidara ya Ufaransa, maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya Uislamu yamefanyika huko Paris, mji mkuu wa nchi hiyo.
-
Marekani; kizuizi kikuu kwa Palestina kuwa mwanachama kamili katika Umoja wa Mataifa
Apr 20, 2024 08:47Marekani ambayo ni muungaji mkono mkuu wa Israel kwa mara nyingine imetumia kura ya turufu (Veto) na kuzuia kupasishwa uanachama kamili wa Palestina ndani ya Umoja wa Mataifa.
-
Mvua kali za mafuriko zaua watu wasiopungua 168 Pakistan na Afghanistan
Apr 20, 2024 07:11Watu wasiopungua 168 wamepoteza maisha katika matukio yaliyosababishwa na mvua, baada ya mvua kali na mafuriko kuikumba Pakistan na nchi jirani ya Afghanistan.
-
UN: Moto wa vita vya Sudan unachochewa na silaha zitokazo nje za wakiukaji wa vikwazo
Apr 20, 2024 07:11Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya Kisiasa na Ujenzi wa Amani, Rosemary Anne DiCarlo ameliambia Baraza la Usalama kwamba vita nchini Sudan vimesababisha "hali mbaya ya kiwango cha kipekee" inayochochewa na silaha kutoka kwa waungaji mkono wa kigeni ambao wanaendelea kukiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa
-
UNICEF: Utawala haramu wa Israel umeua zaidi ya watoto elfu 14,000 wa Gaza
Apr 20, 2024 04:34Msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) amesema kuwa zaidi ya watoto elfu 14,000 wa Kipalestina wameuawa hadi sasa katika mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza huko Palestina.
-
Katibu Mkuu wa UN: Mahesabu mabaya Asia Magharibi yatasababisha janga kwa dunia
Apr 19, 2024 23:29Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametahadharisha kuhusu hali ya sasa katika eneo la Asia Magharibi na kusisitiza kuwa, kosa moja la kimahesabu yumkini likasababisha maafa kwa eneo hilo na dunia nzima kwa ujumla.