Apr 23, 2024 10:24 UTC
  • Waandishi wakosoaji wa Israel wasusia tamasha la jumuiya ya PEN America

Tamasha ya Jumuiya ya Kalamu ya Marekani (PEN America) imefutwa kutokana na ukosoaji mkubwa wa waandishib walioalikwa katika sherehe hiyo dhidi ya jinai na uhalifu unaofanywa na Israel huko Gaza.

Katika barua ya wazi kwa kundi la fasihi na kutetea haki za binadamu la PEN America, waandishi kadhaa mashuhuri wametangaza uamuzi wao wa kususia tamasha la mwaka huu la PEN World Voices wakitaja kushindwa kwa kundi hilo kushughulikia ipasavyo vita vya Israel huko Gaza.

Sehemu moja ya barua hiyo inasema: "Katika muktadha wa vita vya Israel dhidi ya Gaza, tunaamini kwamba PEN America imesaliti dhamira ya shirika hili la kuleta amani na usawa kwa wote, na uhuru na usalama kwa waandishi kila mahali."

Barua hiyo pia inaikosoa PEN America kwa kusitasita kuungana na mashirika mengine ya kutetea haki za binadamu katika wito wa kusitishwa mapigano mara moja huko Gaza.

Katika barua ya wazi iliyochapishwa mwezi uliopita pia, waliotia saini waliikosoa PEN America kwa kutohamasisha "uungaji mkono wowote mkubwa" kwa watu wa Palestina na kwa kutosisitiza dhamira ya taasisi hiyo ya "kupinga chuki za aina zote na kuunga mkono matarajio ya binadamu ya kuishi kwa amani na usawa." 

Hasi sasa jeshi la utawala haramu wa Israel limeua zaidi ya wapalestina elu 34 na kujeruhi wengine zaidi ya elfu 76. 

Tags