Apr 20, 2024 08:04 UTC
  • UNICEF: Utawala haramu wa Israel umeua zaidi ya watoto elfu 14,000 wa Gaza

Msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) amesema kuwa zaidi ya watoto elfu 14,000 wa Kipalestina wameuawa hadi sasa katika mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza huko Palestina.

James Elder amesema katika mtandao wa kijamii wa X kwamba  zaidi ya wasichana na wavulana Elfu 14,000 wa Kipalestina wameuawa huko Gaza. Elder ametoa wito wa kusitishwa mara moja mapigano huko Gaza na kutoa onyo kali dhidi ya utawala vamizi wa Israel unaofanya mashambulizi katika mji wa kusini wa Rafah, ambapo karibu zaidi ya nusu ya wakazi milioni 2.4 wa Ukanda wa Gaza wamekimbilia tafuta hifadhi kutokana na mashambulizi ya utawala haramu wa Israel.

Ujumbe huo wa msemaji wa UNICEF, James Elder kwenye mtandao wa kijamii wa X umekuja kufuatia chapisho la mwandishi wa habari wa Marekani anayefanya kazi na gazeti la The New York Times, ambapo aliashiria ripoti ya CNN kuhusu shambulizi la Israel lililoua watoto wanane waliokuwa wakicheza soka

"Kila dakika 10 mtoto mmoja huuawa au kujeruhiwa huko Gaza, ameripoti Jeremy Diamond," Anne Barnard alisema katika ripoti hiyo.