Apr 23, 2024 03:08 UTC
  • Sunak: Safari za kwanza za ndege kuelekea Rwanda za wanaotafuta hifadhi zitaanza baada ya wiki 10 hadi 12

Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak, ameahidi kwamba safari za kwanza za ndege za nchi hiyo za raia wa nchi mbalimbali wanaotafuta hifadhi zitaanza kuondoka Uingereza kuelekea Rwanda baada ya wiki 10-12.

Waziri Mkuu wa Uingereza ameahidi kumaliza mkwamo uliojitokeza katika bunge la nchi hiyo kuhusu sera ya kuwapatia hifadhi huko Rwanda raia  wanaotafuta hifadhi nchi humo.

Wahajiri wanaotafuta hifadhi 

Sunak alibainisha haya jana katika mkutano na waandishi wa habari baada ya kuahidi wiki iliyopita kuwa bunge la Uingereza litaendelea na vikao vyake hadi kupasishwa muswada katika uwanja huo. 

Waziri Mkuu wa Uingereza amesema kuwa tayari wamekodi ndege kwa ajili ya kuwasafirisha raia watakaopewa makazi huko Rwanda. Rishi Sunak anafanya kila awezalo ili kutimiza ahadi aliyotoa kwa wananchi wa Uingereza ya kuzuia boti zinazoleta wahamiaji nchini Uingereza kinyume cha sheria. 

Mahakama ya Juu ya Uingereza ilisema mwaka uliopita kwamba, mpango wa serikali ya London wa kuwapeleka nchini Rwanda wakimbizi na waomba hifadhi walioko nchini humo unakiuka sheria. Ilisema mpango huo unawaweka katika hali hatarishi wakimbizi hao, hasa kwa kuzingatia kuwa baadhi yao waliikimbia nchi yao ya Rwanda na kuwarejesha huko ni kutawaweka hatarini.

 

Tags