May 02, 2024 07:38 UTC
  • Iran yakaribisha kuendelea mazungumzo kati yake na Umoja wa Ulaya

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekaribisha na kuunga mkono kuendelea kufanyika mazungumzo kati ya Umoja wa Ulaya na Iran ili kusogeza mbele ushirikiano wa pamoja na kusema: Ushirikiano kati ya wakala wa IAEA na Iran upo katika njia nzuri.

Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, Hossein Amir Abdollahian Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekaribisha kuendelea mazungumzo kati ya Umoja wa Ulaya na Iran ili kuendeea ushirikiano wa pande mbili. Abdollahian ameeleza haya katika mazungumzo ya simu na Josep Borrell Mkuu wa Sera za Nje wa EU. 

 Amir Abdollahian amemjibu Borrel kwa kukumbusha juhudi zilizofanywa hadi sasa na hatua chanya zilizochukuliwa na Iran katika diplomasia ya kuondoa vikwazo na kuashiria kupenda makuu kwa baadhi ya pande katika mazungumzo hayo na kuongeza kuwa, ushirikiano kati ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) na Iran upo katika mwelekeo mzuri.  

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran pia ameshiria nafasi na mchango mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) katika kusaidia kudumisha amani na uthabiti katika eneo na kupambana na ugaidi na kuutaka Umoja wa Ulaya kuzingatia suala la kuheshimiwa vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika fremu ya sheria za kimataifa. Abdollahian pia ameeleza kuwa hatua ya Iran ya kuuadhibu utawala wa Israel kufuatia shambulio ulilofanya katika ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus Syria ilikuwa katika fremu ya kujihami halali. 

Vikosi vya IRGC 

Katika mazungumzo hayo ya simu, Josep Borrell Mkuu wa Sera za Nje wa EU pia amesisitiza kuwa umoja huo hautaki kuwa na mivutano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Borrell aidha amekaribisha hatua chanya na athirifu za Iran sambamba na kuendelea kufanyika mashauriano ya kidiplomasia kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Umoja wa Ulaya. 

Tags