Apr 06, 2024 03:10 UTC
  • Jumamosi tarehe 6 Aprili 2024

Leo ni Jumamosi tarehe 26 Ramadhani 1445 Hijria inayosadifiana na tarehe 6 Aprili 2024.

Siku kama ya leo miaka 444 iliyopita, ardhi ya Ureno, moja kati ya nchi zilizokuwa na nguvu barani Ulaya katika karne za 15 na 16 iliunganishwa na Uhispania. Ureno ilikuwa mpinzani wa kisiasa na kikoloni wa Uhispania huko Asia, Afrika na Marekani. Hata hivyo kutokana na raia wa nchi hiyo kuhamia kwa wingi katika nchi makoloni ya Ureno na vile vile hali mbaya ya kiuchumi taratibu Ureno ilianza kupoteza satwa na nguvu yake ya kisasa. Udhaifu na kutokuwa na nguvu Ureno uliipelekea Uhispania kuivamia nchi hiyo. Pamoja na hayo yote hatimaye mapambano ya ukombozi ya wananchi wa Ureno ya mwaka 1640 yalipelekea kukombolewa tena nchi hiyo. 

 

Miaka 106 iliyopita katika siku kama ya leo, serikali ya Marekani ilitangaza vita dhidi ya Ujerumani na ikaingia katika Vita vya Kwanza vya Dunia kwa maslahi ya Waitifaki. Tab'an kabla ya hatua hiyo, Marekani ilikuwa imekata uhusiano wake wa kisiasa na Ujerumani na ilikuwa ikizisaidia nchi Waitifaki. 

Miaka 60 iliyopita katika siku hii, Kufuatia maandamano na mapambano ya wananchi Waislamu wa Iran, Imam Khomeini (RA), mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliachiliwa huru. Alikamatwa na vyombo vya usalama na kupelekwa jela usiku wa manane wa tarehe 5 Juni 1963  baada ya kutoa hotuba ya kufichua dhidi ya utawala wa kiimla wa Shah.  Baada ya wananchi kujua kuhusu kuachiliwa kwa kiongozi wao, sherehe zilifanyika kote nchini Iran.

Imam Khomeini

Miaka 39 iliyopita katika siku kama hii ya leo Ja'far Nimeiry, Rais wa zamani wa Sudan alipinduliwa na Jenerali Abdulrahman Swarul Dhahab aliyekuwa Waziri wa Ulinzi ambaye alichukua madaraka ya kuiongoza Sudan. Ni vyema kuashiria hapa kuwa Nimeiry pia aliingia madarakani kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea Sudan mwaka 1969. Nimeiry aliongoza Sudan kimabavu kwa miaka 16 na kuanzisha uhusiano mkubwa  kati ya nchi hiyo na Marekani.

Ja'far Nimeiry

Na katika siku kama ya leo miaka 30 liyopita, Wahutu wenye misimamo mikali wa Rwanda walianzisha mauaji makubwa dhidi ya Watutsi. Katika mauaji hayo Wahutu wenye misimamo mikali waliwauwa raia wa Kitutsi na Wahutu wenye misimamo ya wastani karibu milioni moja na kuwafanya mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi. Wahutu wanaunda asilimia 84 ya jamii ya Rwanda na kabila hilo lilikuwa madarakani hadi mwaka 1994.

 

 

Tags