-
Marekani yalipigia kura ya veto azimio la kuipatia Palestina uanachama kamili wa Umoja wa Mataifa
Apr 19, 2024 03:59Marekani, ambayo ni muungaji mkono mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, imeendeleza sera yake ya kudhoofisha kupatikana haki za Wapalestina kwa kutumia vibaya haki yake ya kura ya turufu na kukwamisha azimio la kuipatia Palestina uanachama kamili katika Umoja wa Mataifa.
-
New York Times: Israel haikutarajia kabisa kupata majibu makali kama yale kutoka kwa Iran
Apr 18, 2024 23:15Gazeti la New York Times la nchini Marekani limefichua kuwa, ushahidi uliopatikana kutoka kwenye duru za ndani za Israel unathibitisha kuwa Tel Aviv haikutarajia kabisa kupata majibu makali kiasi chote kile kutoka kwa Iran baada ya kuushambulia ubalozi wa Iran mjini Damascus Syria.
-
Galloway akosoa sera za kinafiki za London kuhusu Iran
Apr 18, 2024 08:13Mwanasiasa maarufu wa Uingereza amejibu mashambulizi ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, akihoji: "Kwa nini hukulaani vikali shambulio la Israel kwenye sehemu ya ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus, Syria."
-
Wawakilishi wa Kongresi: Israel inakiuka sheria kwa kutumia silaha za Marekani kufanya mauaji
Apr 18, 2024 07:10Kundi la wawakilishi wa chama cha Demokratic katika Kongress ya Marekani limesisitiza kuwa, utawala wa Israel unakiuka sheria kwa kutumia silaha za Marekani kufanya mauaji na mashambulizi makali huko Palestina.
-
Marekani inawashinikiza kwa siri wanachama wa UNSC wapinge Palestina kuwa mwanachama kamili wa UN
Apr 18, 2024 02:51Marekani inazishinikiza kwa siri nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kukataa ombi la Palestina kuwa mwanachama kamili wa taasisi hiyo kuu ya kimataifa.
-
Borrell: Ukraine isiombe kupewa msaada na Magharibi kama iliopewa Israel katika shambulio la Iran
Apr 18, 2024 02:19Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amesema, Ukraine haipaswi kuomba msaada wa aina ile ile ambayo nchi za Magharibi zilitoa kwa Israel wakati wa shambulio la kijeshi la Iran kwa sababu hali hizo mbili haziwezi kulinganishwa.
-
Wabunge Uingereza waitaka serikali isitishe kuiuzia silaha Israel
Apr 18, 2024 01:03Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza imepokea waraka wa maombi wenye jumla ya saini lfu 70 zikiwemo saini za baadhi ya wawakilishi wa Bunge la nchi hiyo wanaotaka kusitishwa kutumwa mabomu na makombora ya nchi hiyo kwa Israel.
-
Rais wa Uturuki: Israel imempiku Hitler kwa kuua watoto 14,000 wasio na hatia Ghaza
Apr 17, 2024 07:41Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema, Israel tayari imempiku kiongozi wa Wanazi Adolf Hitler kwa kuua zaidi ya watoto 14,000 wasio na hatia katika Ukanda wa Ghaza.
-
NYT yaagiza waandishi wake: Msitumie misamiati ya 'mauaji ya kimbari', 'uangamizaji wa kizazi' katika vita vya Israel
Apr 17, 2024 07:18Taasisi ya uchunguzi wa taarifa za mitandaoni nchini Marekani ya Intercept imefichua kuwa gazeti la New York Times limewaagiza waandishi na maripota wake wa habari wanaoripoti vita vya mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza, wajizuie kutumia misamiati ya "mauaji ya kimbari" na "uangamizaji wa kizazi" na kupeuka kutumia neno “eneo linalokaliwa kwa mabavu” kumaanisha ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Israel.
-
Kikao cha Baraza la Usalama: Uwanja wa makabiliano kati ya waungaji mkono wa Iran na Wamagharibi wanaounga mkono utawala wa Kizayuni.
Apr 16, 2024 04:24Kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kujadili mashambulizi ya Iran ya kuuadhibu utawala wa Israel kilifanyika Jumapili jioni tarehe 14 Aprili, kikao ambacho kilibadilika na kuwa uwanja wa makabiliano kati ya nchi zinazounga mkono Iran na kambi ya Magharibi waitifaki wa utawala wa Kizayuni.