-
Rais wa zamani wa Korea Kusini afungwa maisha jela
Feb 19, 2026 23:56Mahakama ya Korea Kusini jana Alkhamisi ilimhukumu rais wa zamani wa nchi hiyo, Yoon Suk Yeol kifungo cha maisha jela kwa kutangaza sheria ya kijeshi mnamo Desemba 2024, na kumtia hatiani mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 65 kwa kuongoza uasi na kuhujumu katiba.
-
Waholanzi 640 waliohudumu katika jeshi la Israel Gaza kushtakiwa?
Feb 19, 2026 23:56Zaidi ya raia 640 wa Uholanzi wamehudumu katika jeshi la Israel wakati wa vita vya mauaji ya halaiki vya utawala huo wa Kizayuni dhidi ya Gaza na kwneye mashambulizi dhidi ya Ukingo wa Magharibi, takwimu mpya zinaonyesha, huku wataalamu wa sheria wakionya kwamba, wale waliohusika wanaweza kushtakiwa chini ya sheria za kimataifa na za nchi hiyo za uhalifu wa kivita.
-
Kinachovifanya vyama vya Kiislamu vya Pakistan vipinge nchi hiyo kuwemo kwenye 'Bodi ya Amani' ya Trump
Feb 19, 2026 23:55Shinikizo la kisiasa la vyama vikuu vyenye mielekeo ya Kiislamu nchini Pakistan kwa serikali ya nchi hiyo la kuitaka ijiondoe katika kile kiitwacho 'Bodi ya Amani' ya Trump limeongezeka.
-
Uzandiki na undumakuwili wa wazi wa Marekani katika sera yake ya kurutubisha urani
Feb 19, 2026 07:16Waziri wa Nishati wa Marekani amesema, nchi hiyo itaanza tena kurutubisha madini ya urani
-
Vatican, Mexico nazo pia zaukataa uanachama katika 'Bodi ya Amani' ya Trump
Feb 18, 2026 07:00Vatican haitashiriki katika mpango wa Rais wa Marekani Donald Trump wa iitwayo "Bodi ya Amani". Hayo yameelezwa na afisa mkuu wa kidiplomasia wa Vatican Kardinali Pietro Parolin, huku akisisitiza kwamba juhudi za kushughulikia hali za mgogoro inapasa zisimamiwe na Umoja wa Mataifa.
-
Waziri Mkuu wa Slovakia: EU iko katika hali mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia yake
Feb 18, 2026 06:56Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico ameonya kwamba Umoja wa Ulaya (EU) sasa hivi unakabiliwa na hali mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia yake, huku matatizo ya kiuchumi yakizidishwa na kukosekana uongozi na maono ya muda mrefu huko Brussels.
-
Baadhi ya Waislamu waanza funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani
Feb 18, 2026 02:54Baadhi ya nchi za Waislamu na Kiarabu zimetangaza leo Jumatano kuwa siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
-
Kremlin: Jeshi la majini la Russia kuzima 'uharamia' wa Magharibi
Feb 18, 2026 02:54Afisa mwandamizi wa Ikulu ya Russia (Kremlin) ameonya kwamba, yumkini jeshi la wanamaji la nchi hiyo likatumwa kuzuia mataifa ya Magharibi kukamata meli za Urusi kama sehemu ya vikwazo dhidi ya usafirishaji wa mafuta ya Moscow.
-
Wataalamu wa UN waonya kuhusu hatari zinazowakabili waathirika wa "Mafaili ya Epstein"
Feb 17, 2026 23:35Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wamesema, wana wasiwasi mkubwa kuhusu madhara yanayoweza kuwapata waathirika waliotajwa katika nyaraka zinazojulikana kama "Mafaili ya Epstein" (Epstein Files), na kueleza kwamba mchakato wa utoaji wa taarifa hizo haukulinda ipasavyo faragha na usalama wao.
-
UN yatoa wito mpya wa kutokomeza ukoloni
Feb 17, 2026 07:09Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema ingawa zaidi ya mataifa 100 yamepata uhuru tangu mwaka 1945, mchakato wa kuondoa ukoloni bado haujakamilika. Ametoa kauli hiyo akifungua kikao cha mwaka 2026 cha Kamati Maalum ya Umoja wa Mataifa kuhusu Kutokomeza Ukoloni,