Sep 26, 2023 07:35 UTC
  • Burkina Faso yalifungia jarida la Kifaransa kwa kujaribu kulifanyia dharau jeshi

Watawala wa kijeshi wa Burkina Faso wameagiza kusitishwa usambazaji wa jarida linalochapishwa kwa lugha ya Kifaransa la "Jeune Afrique" likituhumiwa kuwa limekuwa likijaribu kushusha hadhi ya jeshi la nchi hiyo.

Serikali ya Burkina Faso imekosoa makala mpya na ya kupotosha iliyochapishwa jana na jarida hilo la lugha ya Kifaransa chini ya anwani "Mvutano unaendelea katika jeshi la Burkina Faso". Makala hiyo tajwa inafuatia ile ya huko nyuma iliyochapishwa na jarida hilo la lugha ya Kifaransa katika tovuti moja Alhamisi iliyopita. Jarida la Jeune Afrique lilidai kuwa malalamiko yanazidi kuongezeka katika kambi za jeshi nchini  Burkina Faso. 

Watawala wa kijeshi wa Burkina Faso wameeleza katika taarifa yao wakijibu hatua ya jarida la Jeune Afrique kuwa: "Madai haya ya kimakusudi yaliyotolewa bila uthibitisho hayana lengo jingine ghairi ya kulifanyia dharau jeshi la taifa. 

Watawala wa kijeshi wa Burkina Faso 

Itakumbwa kuwa mwezi Juni mwaka huu uongozi wa Burkina Faso ulitangaza kusitisha matangazo ya televisheni ya Kifaransa ya LCI kwa miezi mitatu baada kuwafukuza nchini waandishi wa magazeti ya kila siku ya Ufaransa ya Liberation na Le Monde mwezi Aprili.

Tags