Feb 21, 2024 02:20 UTC
  • Zaidi ya nusu ya nchi 20 zenye uchumi unaostawi kwa kasi zaidi duniani 2024 ni za Kiafrika

Afrika itachangia nchi 11 kati ya 20 zinazokua kwa kasi kiuchumi duniani mwaka 2024. Hayo ni kulingana na ripoti ya hivi punde ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

Nchi 11 bora za Afrika zinazotarajiwa kuwa na ukuaji wa juu zaidi wa Pato la Taifa (GDP) ni Niger (11.2%), Senegal (8.2%), Libya (7.9%), Rwanda (7.2%), Côte d'Ivoire (6.8%), Ethiopia (6.7%). %), Benin (6.4%), Djibouti (6.2%), Tanzania (6.1%), Togo (6%), na Uganda (6%).

Aidha, ripoti hiyo imebaini kuwa nchi 41 barani humo zitafikia kiwango cha ukuaji wa uchumi wa 3.8% mwaka 2024, huku 13 kati yao zikiongezeka kwa zaidi ya asilimia 1 kwa kasi zaidi kuliko mwaka 2023.

Ulimwenguni, benki hiyo ilitabiri kuwa Afrika itasalia kuwa eneo la pili kwa kukua kwa kasi baada ya Asia, huku ukuaji halisi wa Pato la Taifa (GDP)  katika bara hilo ukiwa wastani wa 3.8% na 4.2% mwaka 2024 na 2025, mtawalia. Ustawi huo wa kasi wa uchumi wa Afrika ni  juu ya makadirio ya wastani ya kimataifa ya 2.9% na 3.2%.

Ikitoa taswira ya kikanda ya bara hili, AfDB iliangazia Afrika Mashariki, ambayo ukuaji wake unatarajiwa kupanda hadi 5.1% mwaka 2024 na 5.7% mwaka 2025.

Benki hiyo pia ilipendekeza kuwa bara la Afrika linapaswa kuwekeza zaidi katika mtaji wa watu na kufuata mkakati wa uanzishaji wa viwanda unaozingatia rasilimali na mseto wa sera ambazo zitaruhusu bara hili kujenga uwezo wa kustahimili majanga.

 

Tags