Wazazi Nigeria waungana na watoto wao waliokuwa wametekwa nyara
(last modified Thu, 28 Mar 2024 07:02:55 GMT )
Mar 28, 2024 07:02 UTC
  • Wazazi Nigeria waungana na watoto wao waliokuwa wametekwa nyara

Wazazi wa watoto wa shule zaidi ya 130 nchini Nigeria wamekombolewa kutoka mikononi mwa watekaji nyara baada ya kushikiliwa mateka kwa zaidi ya wiki mbili. Wazazi hao jana waliungana na watoto wao; ambapo walishindwa kuzuia machozi ya furaha katika tukio hilo walilokuwa wakilisubiri kwa muda mrefu.

Tukio la kukutana wazazi na watoto hao tajwa lilifanyika jana katika jengo moja la serikali katika mji wa Kaduna siku tatu baada ya watoto hao kukombolewa. Watoto hao wa shule hivi sasa wanaishi hapo wakiendelea kupatiwa huduma ya afya na matibabu. 

Wazazi wamesema kuwa waliungana tena jana na watoto wao kwa mara ya kwanza tangu Machi 7 mwaka huu wakati watu waliokuwa na silaha wakiwa kwenye pikipiki walipowateka nyara shuleni kwao katika mji wa Kuriga kaskazini magharibi mwa jimbo la Kaduna na kuwalazimisha kuongozana nao hadi katika misitu ya karibu huku wakifyatua risasi.   

Watoto wa shule waliotekwa nyara mara baada ya kukombolewa

Shittu Abdullahi mzazi wa mwanafunzi binti mwenye miaka 14 aliyekuwa ametekwa nyara amesema kuwa amefurahi sana kujumuika tena na mtoto wake."

Wakati huo huo maafisa wa jeshi la Nigeria wamesema kuwa mfanyakazi mmoja wa shule ambaye alitekwa nyara pamoja na wanafunzi hao 137 aliaga dunia mikononi mwa watekaji nyara. 

Serikali na jeshi la Nigeria linaendelea kuwapatia matibabu na huduma ya afya watoto hao wa shule ambao walikombolewa na jeshi  Jumapili iliyopita kutoka katika msitu umbali wa kilomita zisizopungua 200  kaskazini katika jimbo jirani la Zamfara.